Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, July 2, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAONYESHO YA 35 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR….!!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa , wakati alipotembeleea maonyesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam, Julai 01, 2011.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikata utepe kuzindua, Redio Sibuka FM.
Pichani Juu na Chini ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akitoa burudani na Bendi yake mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzizi wa maonyesho hayo Julai 01, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi wa jumla Mkurugenzi Mkuu NSSF, Dkt Ramadhan Dau, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.


Ramadha Dau, akifurahia tuzo yake baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF, wakifurahia kwa pamoja na tuzo yao.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi wa kundi la Engineering Priducts, Mkurugenzi Mkuu wa Sido, Mike Laiser, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi mwakilishi wa Home Shoping Center. wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Ramadhan Hashim Khalfan, baada ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, uliofanyika Julai 01, 2011 kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Mwakilishi wa SBL, akiwa na tuzo yake baada ya kukabidhiwa kama wadhamini wakuu wa kinywaji cha maonyesho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoka nje ya banda la Maliasili na Utalii, wakati akikagua mabanda ya maonyesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula, wakati alipotembelea na kukagua Banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa, baada ya Makamu kuzinduz maonyesho hayo rasmi Julai 01, 2011. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Mark Wiessinga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessinga, wakati alipotembelea na kukagua Banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa, baada ya Makamu kuzindua maonyesho hayo rasmi Julai 01,2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikagua bidhaa za Delphine Mlambiti wa Blessing Fashion Centre wakati akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB akikagua mabanda ya maonyesho. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Mark Wiessinga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya Banda la Mjasiliamali wakati alipotembelea Banda la benki ya NMB. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

No comments: