Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 31, 2011

Dodoma mabingwa wa pool taifa 2011

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kulia) akikabidhi kombe la ubingwa wa Taifa wa Mashindano ya Safari Lager kwa Nahodha wa Timu ya Pool ya mkoa wa Dodoma ambao ndio mabingwa wapya wa mchezo huo kwa mwaka huu.
Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni zawadi ya ubingwa wao huo walioupata usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 3.5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Ilala,ikiwa zawadi ya ushindi wa pili walioupaka mkoa huo.

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Safari Lager Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene akiwa pamoja na viongozi wa mchezo wa Pool na viongozi wa TBL wakifuatilia moja ya michezo ya Fainali za Pool za Taifa kati Ilala na Dodoma iliyokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Kilimani,Mjini Dodoma Usiku wa Kuamkia leo.
Kuona picha Zingine
Habari kwa hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog

No comments: