Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 31, 2011

Latest News: MEYA WA SONGEA AFARIKI DUNIA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Ali Saidi Manya, Diwani wa kata ya Lizaboni(Mwenye suti Nyeupe) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Misheni Peramiho.

Taarifa za Msiba huo zimetangazwa na naibu Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Mariam Dizumba na kupokelewa kwa mshtuko mkubwa na wakazi wa manispaa ya Songea Mkoa wa ruvuma kwa ujumla.

Naibu Meya Dizumba amesema mazishi ya Mstahiki Meya Ali Saidi Manya yatafanywa nyumbani kwake Lizaboni Manispaa ya Songea Siku ya Jumatatu Tarehe 1 Agosti 2011. Maandalizi yanaendelea na wageni kadhaa wa vyeo mbalimbali wamethibitisha kuhudhuria.

Mtandao huu unaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahale pema peponi

No comments: