Asha Salimu ambaye ni muongozaji wa michezo ya filamu na ya jukwaani akimueleza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) umuhimu wa wasanii kupewa elimu zaidi ili waweze kufanya kazi zao vizuri. Waziri Dk. Nchimbi alikutana leo na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali wakinyosha vidole ili kupata nafasi ya kumuuliza maswali Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) kuhusu matatizo yanayowakabili. Waziri Dk. Nchimbi alikutana leo na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Muigizaji wa picha nyongefu Hemedi Maliyaga maarufu kama “Mkwere” akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) nakala ya DVD ya Mstaafu aliyoiandaa hivi karibuni yeye pamoja na wasanii wenzake wa kundi la Kashi-kashi Arts Groups wakati waziri huyo alipokutana na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu ili kujua matatizo yanayowakabili katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kazi zao kwa jamii katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni naibu waziri wa wizara hiyo Dk. Fenella Mukangara na kushoto ni Rashidi Masimbi ambaye ni mjumbe wa BASATA.
Muigizaji wa picha nyongefu Hemedi Maliyaga maarufu kama “Mkwere” akijitambulisha jina lake mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati waziri huyo alipokutana na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu ili kujua matatizo yanayowakabili katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu jinsi Serikali inavyoshughulikia matatizo mbalimbali yanayowakabili. Waziri Dk. Nchimbi alikutana leo na wasanii hao katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Muigizaji wa picha nyongefu Emmanuel Myamba akimueleza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) jinsi ambavyo Serikali inakosa mapato kutokana na kazi za wasani. Waziri Dk. Nchimbi alikutana leo na wasanii wa sanaa za ufundi, maonyesho na picha nyongefu ili kujua matatizo yanayowakabili katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala jijini Dar es Salaam.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment