Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 16, 2011

mbunge amtembelea mama anayezaa kiajabu arumeru leo

Mbunge wa Viti Maalumu Vijana CCM) Mh. Catherine Magige, leo ametembelea kijiji cha Maji ya Chai Wilayani Arumeru na kumsaidia mwanamke mwenye uzazi wa ajabu, Bi Chausiku Suleimab, ambaye anabeba mimba kwa miaka mitatu na hivi sasa ana watoto 18. Vile vile ana mimba nyingine iliyodumu miaka 3.

Mh. Magige amempatia msaada Mama huyo kwenda Loliondo kwa Babu, amemlipia kodi ya nyumba kwa mwaka mmoja, pamoja na kuta ada ya shule kwa watoto wake watano.


Mh. Magige pia alitembelea Magereza na kuongea na wafungwa ambako alijitolea kuwalipia wafungwa zaidi ya 10 fedha za faini ili waachiwe huru. Wafungwa wamemshukuru sana Mbunge huyu kijana kwa kuwatembelea.

Bi Chausiku Sulemani Mkazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru anayezaa bila kupumzika na kila akizaa anaacha mtoto mwingine tumboni baada ya ujauzito wa miaka mitatu
Bi Chausiku akilia kwa uchungu wakati akielezea mateso yake ya zaidi ya miaka 15 ya kuzaa bila kupumzika huku akiwa hajakutana na mume wake kimwili
Mbunge wa Viti maalumu Mh. Catherine Magige akimpatia
msaada Bi Chausiku huku watoto wake wakiwa mamemzingira

Mh. Catherine Magige akiwa amempakata mmoja wa watoto wa Bi Chausiku
Mh. Catherine Magige akiwa anatoka nyumba ya kupanga
ya chumba kimoja anayoishi Bi Chausiku na watoto wake 18
Picha na maelezo kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments: