Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina Elekezi kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali, mjini Dodoma.Kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Kulia ni Jaji Mkuu, Othman Chande.
Baadhi ya washiriki wa Semina Elekezi kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali,wakiwa nje ya ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma, baada Rais Jakaya Kikwete kufungua semina hiyo
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta na Waziri Mkuu, Mstaafu Mh. Cleopa David Msuya kwenye viwanja vya Kituo cha mikutano cha St. Gaspar Mjini Dodoma leo wanakohudhuria Semina Elekezi.
Baadhi ya washiriki wa Semina Elekezi kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali,wakiwa nje ya ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma, baada Rais Jakaya Kikwete kufungua semina hiyo.,Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Salum Shamte (kushoto) akiteta jambo na Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya wakati wa semina hiyo.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman (wa pili kushoto), akizungumza na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa wakati wa semina hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika semina elekezi,. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema na Kamishna wa Magereza, Augustino Nanyaro.
Picha zote na Kamanda wa Matukio Richard Mwaikenda
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog
"
No comments:
Post a Comment