Baadhi ya Abiria na wananchi ambao walifika eneo hilo la tukio kushuhudia kimbembe hicho maeneo ya mwenge ambapo Dereva aligoma kuwapeleka abiria Mbezi Kimara
Traffic akiwa amefika eneo la tukio baada ya kupewa malalamiko na moja ya abilia katika eneo hilo
Break down likiwa tayali eneo la tukio baada ya dereva wa gari hilo kugoma kuwasafikisha abiria na kutaka kuchukua Gari hilo kulipeleka eneo husika
Dereva wa Basi hilo akipokea kipondo cha nguvu na Traffic aliye nusulika kuuawa.
--------
"Unataka kuniuwa wewe" alisikika Traffic huyo ambae alinusurika kifo jana usiku majira ya sa mbili na nusu. katika hali isiyo ya kawaida dereva wa basi ambalo linaenda Muhimbili/Mbezi kuvunja sheria na kupaki maeneo ya mwenge na kudai kuwa anaelekea mpaka Kimara na kudai hafiki Mbezi kama ilivyo andikwa, baada ya abiria kulalamika sana ndipo dereva na konda wake wakashuka na kusema hawata fanya tena safari hiyo na kuwasihi abiria wapande Gari zingine, lakini abiria hao walikomaa na kugoma, Baada ya muda wa takribani dakika 30, abiria mmoja alitoka na kwenda kutoa taarifa kwa trafiki ambae alikuwa maeneo hayo ya jirani kumweleza tatizo na alipo fika eneo hilo akamkuta konda tuu bila dereva alipo uliza dereva yuko wapi alijibiwa kuwa ametoka anakuja, Mwana usalama huyo wa barabarani alipo ona jamaa haji ikabidi aite Break down kunyanyua gari hilo na kupeleka kituoni. Ndipo dereva alijitokeza na jugomea swala hilo "Gari hii nasema haiendi kokote kule na mnataka kuchukua kwa kisa gani?" aliongea dereva huyo na kusema kwamba "Kama kukataa ni mimi nimekataa kwa hiyo niacheni talipeleka mwenyewe kituo cha Polisi" alipo maliza alipanda kwa Gari halaka halaka na kutaka kukimbia, Traffic alipo ona jamaa anataka kuondoka ndipo alienda mbele na kuzuia asiendelee na safari zake lakini hata hivyo dereva huyo alizidi ongeza mwendo na kutaka kummaliza Traffic huyo,na kwa bahati nzuri kulikuwa na Gari mbele zikazuia. Dereva alipo ona hali ni tete akachomoka katika usukani na kuanza kukimbia lakini Mbio za sakafuni hakufika mbali na akakamatwa na Traffic huyo huyo aliye taka kumuua. Hata hivyo alipokea kichapo cha nguvu na kupelekwa kituoni. Baada ya hapo Kamera yetu iliendelea na kazi zingine.
No comments:
Post a Comment