Hili ndilo eneo kama linavyo onekana ambapo mtu huyo anae jiita muwekezaji amevamia na kujenga
Uzio ambao umewekwa na anae jiita muwekezaji Ndugu Msaki
Baadhi ya Majengo yake
Hapa ni uzio huo unao onekana kwa ukaribu ambapo watoto walikua wakicheza hapo na sasa imebaki kuwa Historia
Mafundi wakiendelea na ujenzi katika eneo hilo ambapo kimsingi ni eneo la watoto kucheza
Wakiwa wanaendelea Kuporomosha majengo eneo hilo ambalo si la ujenzi
Pichani si sehemu ya ramani, ya kitalu namba 4 aliyo na usajili na 38383, E' 353/107 toleo la tarehe 24/05/2004 inayoonyesha kuwa kiwanja no 30 ni eneo la wazi.
Eneo la mivumoni limekubwa na wawekezi katika maeneo ya wazi, Pichani ni kiwanja na 30 chilichopo kitalu namba 4,kikiwa kimezungushiwa uzio na mwekezaji aliyejulikana kwa jina moja la Msaki. Wakazi ya maeneo halo walifanya usafi wa eneo ili kuwawezesha watoto kucheza mpira wa miguu ndipo mwekezaji huyo alipojitokeza akajenga uzio. Kwa mujibu wa meelezo yake yeye ni mmiliki halali wa eneo hilo.
2 comments:
watanzania tuweni na fikra endelevu haya mambo ya kuvamia Maeneo ya wazi ni ubumbuwazi miaka 20 ijayo kwa akili yako watoto zetu watacheza wapi?Mh.Tibaijuka huyu msaki sidhani kama ni kikwazo kwa wewe kufanya maamuzi ya busara kama yale ya pale Blue palms na Ocean road...............bloger link na kwa mabloger wenzako hizi issue kwa mfano Issa Michauzi, Michuzi Junior , Lady Jaydee na wengine ili mambo kama haya yasitishwe - Mdau CMN.
huyu jamaa sijui kapata wapi nguvu yaani hata mjumbe wa nyumba kumi alizarau na isitoshe akatumia silaa kutishia wananchi. Tunaamini uongozi wa ardhi watachukua uamuzi haraka maana kila nikipita roho inauma
Post a Comment