Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 9, 2011

Kule kule Gizani kuanzia 19.05.2011

Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, limetangaza upungufu mkubwa wa umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia Mei 19 hadi 26 ili kutoa nafasi ya matengenezo makubwa katika visima vya gesi ya Songo Songo.

Mgao huo mkubwa utainyima nchi umeme kwa saa 16 katika kipindi cha saa 24 kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi William Mhando alisema mgao unatokana na kusimamishwa kwa uzalishaji wa gesi asili iliyopo katika Kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na wamiliki wa visima hivyo Pan African Energy Tanzania Limited, wakiwa na lengo la kuvifanyia ukaguzi na ukarabati ili kuboresha uzalishaji wa gesi kwa ajili ya kufulia umeme.

Tangu mwanzo wa mwaka jana gesi inayotolewa na kusafirishwa Dar es Salaam kwa matumizi ya umeme na viwanda imekuwa ikipungua kutokana na sababu za kiufundi.

Kutokana na kuzimwa kwa visima hivyo, vituo vya Songas, Ubungo Gas Plant na Tegeta Gas Plant vinavyotumia gesi asilia kufua umeme vitasitisha shughuli zake kwa siku hizo nne na hivyo kusababisha upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa kwa sababu umeme wa gesi huchangia karibu nusu ya umeme unaofuliwa katika vituo vyote nchini.

Mhando alisema kuanzia Mei 23 - 26 mchana, mgao wa umeme utakuwa megawati 300 kuanzia saa 2 asubuhi - saa 5 usiku na megawati 50 kuanzia saa 5 usiku - saa 2 asubuhi.

Kuhusu nishati ya maji, shirika hilo limesema hali ya umeme imekuwa nzuri siku za karibuni kutokana na mvua zilizonyesha na kuongeza maji kwenye vituo vya Kihansi, Kidatu na Pangani na kuwezesha uzalishaji umeme katika vituo hivyo na kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa muda.

Hata hivyo, Mhando alisema kina cha maji katika Bwawa la Mtera bado kipo chini sana kwani hadi kufikia juzi kina cha maji katika bwawa hilo kilikuwa mita 691.18 usawa wa bahari wakati kina cha juu kwenye bwawa hilo ni mita 698.50 na kina cha chini ni mita 690.00 juu ya usawa wa bahari, hivyo tangu mvua zianze zimeongezeka sentimita 30 tu.

Chanzo: WAVUTI

No comments: