Kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi ya Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu huu 2011, baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza, mchezo ulichezwa kwnye Uwanja wa Kirumba, magoli hayo yakiwekwa kimiani na David Mwape aliyefunga 2 na Nurdin Bakar aliyefunga 1, huku Watani wao wa Jadi Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi yao na Majimaji ya Songea katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imetwaa ubingwa huo kwa tofauti ya kagoli kamoja tu!, na kumvua ubingwa mtani wake wa jadi Simba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment