HAPA ZAMANI PALIKUA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI PALIJULIKANA SANA KWA JINA LA LEGICO KWA SASA NI SHULE YA SEKONDARI LEGICO IPO MAJENGO |
LEGICO SEC |
HUKU NI MAJENGO MTAA WA JOKA ROAD |
JAMANI MBATA PRIMARY SCHOOL MNAIKUMBUKA? |
HII NI MOJAWAPO YA MITAA YA MBATA JUU |
6 comments:
Asante sana kwa hii kumbukumbu ya Shule ya Msingi Mbata. Nilisoma hapo miaka saba. Nilipokuwa darasa la 6 (1988) nilianza kudakia timu ya Shule. Upinzani wetu na timu ya Shule ya Majengo ilikuwa kama Simba na Yanga. Sijui siku hizi kama mechi hizo zipo. Enzi hizo palikuwa hapatoshi. Bila kuwasahau vibonde wetu timu ya Iziwa. Itabidi nitembelee shule yangu na watoto wangu. Wajue nilikotoka. Manake watoto wa siku hizi wamezoea basi la shule kuwafuata mpaka mlangoni.... SJM
ASANTE KESHO TUTAKUONYESHA PICHA YA SHULE YA MSINGI MAJENGO
Duh! Legico siku hizi ni shule. Enzi hizo ilikuwa kilabu maarufu ya pombe za kienyeji (zile za ku-dunk). Watu wengi sana walipotezea mwelekeo wa maisha hapo! Hii ni mfano wa kuigwa kubadili kilabu cha pombe na kufanya shule. By the way kwa wale wasiojua: LEGICO ni neno linalotokana na Legislative Council. Hilo jengo lilijengwa toka enzi za ukoloni na hapo ndipo sheria ndogondogo za wakati huo zilitungwa na kutumika. Endelea kutumwagia hizo kumbukumbu za jiji letu la Mbeya. Sisi huku mbali tunaburudika sana tunapoona picha kama hizo!!
asanteni tutazidi kuwaletea matukio ya picha za mbeya kila mara
mimi ninachanganya kidogo,hivi kulikuwa na shule ya msingi majengo juu na chini,na je mbata ilikuwa karibu na mitaa ya ghana,naomba msaada administrator wa mbeya yetu.
majengo juu kwa sasa haipo mpaka majengo yake waliyatoa ikaanzishwa shule ya maendeleo jirani na mashine ya mwalalika
Post a Comment