Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimollo :
Na Mwandishi wetu Danny Tweve
Taarifa zilizoufikia mtandao wa Indaba Africa pamoja na mtandao dada wa Mbeya yetu zinaeleza kuwa Mzungu mmoja anayefanya kazi kama mtaalam kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Tunduma- Sumbawanga amefariki dunia katika hotel ya Imperial Inn akiwa na shehena ya Unga!.
Taarifa kutoka vyanzo vya muhimu zinaeleza kuwa mzungu huyo amegundulika jana alfajiri baada ya kuchelewa kuamka.
Imeelezwa kuwa mzungu huyo anayejulikana kwa jina la Philip amekutwa amekufa huku kukiwa na unga pembeni mwake na kwamba kilikuwa kileo chake cha siku nyingi na mara kwa mara amekuwa akijidozi kupata stimu ya kupumzikia usiku.
Raia wa Botswana ambaye alikuwa akiishi Afrika kusini, ameishi kwenye hoteli hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu sasa na kwamba juzi alionekana afya yake ikiwa ya kusumbua (kuumwa) lakini aliendelea kujibandika midozi ya unga ambayo inadaiwa imechangia kumtoa roho.
Imeelezwa kuwa kulikuwa na mvutano wa kumfanyia uchunguzi (post mortam) ambapo wazungu wenzake hawakutaka afanyiwe uchunguzi huo kwa kukwepa aibu ya kuonekana mgeni huyo labda alijiover doze! lakini mkuu wa wilaya ya Mbozi alisisitiza ni muhimu mgeni huyo afanyiwe uchunguzi ili kuepusha uwezekano wa baadaye kuzungumzwa mengine juu ya Tanzania, na hususani Mbozi kama ambavyo imekuwa ikitajwa kwenye sifa za matukio tukio!!!
Mengi tutawapasha zaidi baada ya kukamilisha ufuatiliaji wa kifo hicho.
No comments:
Post a Comment