Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mbeya mjini ya CCM,Charles Mwakipesile akichangia jambo wakati Umoja wa Vijana wa CCM wakitoa tamko la kumpongeza Naibu Spika. |
Mjumbe mstaafu wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mbeya mjini CCM, Mama Mwaipasi akitoa ya moyoni kuhusu kinachoendelea bungeni mjini Dodoma kwa Wabunge wa upinzani kususia vikao vya bunge |
Baadhi ya Wanachama wa CCM Mkoa wa Mbeya wakifuatilia tamko likisomwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya na Songwe. |
TAMKO LA UVCCM MKOA WA
MBEYA & SONGWE KUMPONGEZA MHE. DR. TULIA ACKSON MWANSASU (MB) NAIBU SPIKA
WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA 13/6/2016.
TANZANIA 13/6/2016.
Ndugu
wana habari na watanzania mnao tufuatilia kupitia redio na televisheni tupo
hapa mbele yenu kwa lengo mahususi la kumpongeza Mhe. Dr. Tulia Ackson Mwansasu
(MB) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri
anayo ifanya katika kuliongoza na kulisimamia Bunge letu la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa umahiri na ueledi na wa hali ya juu.
Watanzania
wote ni mashahidi kwa namna ambavyo Mhe. Dr. Tulia Mwansasu anavyo lisimamia na
kuliongoza Bunge letu kwa kuzingatia sheria, kanuni, na maadili ya Bunge na
hivyo kurejesha heshima, nidhamu na uwajibikaji kwa Wabunge katika utekelezaji
wa majukumu yao ya kuwawakilisha wananchi.
Kwa
mfano hivi karibu tumeshuhudia akitoa mwongozo wa kutokulipwa fedha Wabunge
wanaoingia Bungeni na kutoka mara tu baada ya kujisajili pasipo kutimiza wajibu
wao hasa kwa kuzingatia kuwa HAKI na WAJIBU vinakwenda pamoja.
Vile
vile kipekee kabisa na kwa umuhimu mkubwa UVCCM Mkoa wa Mbeya & Songwe
tunapenda kumshukuru Mhe. Rais wetu Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe. Dr, Tulia Mwansasu (MB) kuwa Mbunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha kuteuliwa na CHAMA CHA
MAPINDUZI kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na baadaye kuaminiwa kwa kuchaguliwa na Waheshimiwa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura nyingi na za
kishindo.
Sanjali
na hivyo tunapenda kumpongeza Mhe. Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Magufuli
kwa hatua mbali mbali anazo endelea kuzichukua katika kutuletea Maendeleo
Wananchi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kupiga vita rushwa kwa vitendo. Pia
tunawashukuru na kuwapongeza sana Waheshimiwa wabunge wote wanao tokana na
CHAMA CHA MAPINDUZI Kwa Kazi kubwa wanayo endelea kuifanya katika kuisimamia na
kuishauri serikali ,UVCCM Mbeya & Songwe tunawashukuru sana kwa namna ya
kipekee wanavyo endelea kumpatia ushirikiano wa kutosha Mhe. Rais wetu mpendwa
na Mhe, Naibu Spika wetu Mungu awabariki.
Tunasikitishwa
na kulaani vikali vitendo vinavyo fanywa na Wabunge wa Upinzani vya kutaka
KUMHUJUMU Mhe, Naibu Spika kwa sababu zao binafsi zisizo na maslahi kwa Umma
isipo kuwa kwa vyama vyao pekee kwani huwezi kumuundoa Mhe, Naibu Spika kwa
kusimamia kanuni na taratibu zilizo tungwa na wao wenyewe waheshimiwa Wabunge
na kuwanyima wananchi walio wachagua haki yao ya msingi ya kuwawakilisha kwa
kususia vikao vya Bunge kwa kisingizio cha kutokuwa na IMANI na Naibu Spika ili
hali lengo lao ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kuendeleza mizaha na siasa
zisizo na tija kwa Taifa letu ndani ya Bunge kwani nidhahiri kuwa hivi sasa
Wapinzani wamekosa Ajenda za kuzisimamia baada ya vyama vyao kuwakaribisha na
kuwakumbatia Mafisadi pia kwa kazi nzuri inayofanywa na Mhe, Rais ya kutatua
kero za Wananchi kwa kiwango kikubwa. Na zaidi sifa, uwezo na uweledi alionao
Mhe, Naibu Spika Dr. Tulia Ackson Mwansasu vinavyomuwezesha kulisimamia na
kuliongoza Bunge kikamilifu ikumbukwe Mhe, Dr, Tulia Ackson Mwansasu ni msomi
na mbobezi wa sheria kwa kuzisoma, kuzifundisha, kuziandika na kuzifanyia kazi
hivyo Mhe, Naibu Spika anachokifanya ni kuzisimamia na kuzitekeleza sheria na
kanuni za Bunge zilizotungwa na Bunge na hakuna kanuni mpya alizokuja nazo Mhe,
Naibu Spika, kama Wapinzani wanavyotaka kuwaaminisha Wananchi.
UVCCM
Mbeya & Songwe tunasema Usirudi nyuma Mhe. Dr. Tulia Ackson Mwansasu
watanzania wengi tupo nyuma ya kazi yako njema na yenye maslahi kwa Taifa.
RAI YETU KWA WAPINZANI.
Tunawashauri Ndugu zetu wa upinzani kurejelea maneno ya busara tuliyo kumbushwa hivi karibuni na Waziri wa sheria na katiba Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (MB) kutoka kwa Mwana falsafa nguli wa Ugiriki “PLATO” aliye pata kusema “wenye busara husema wanapokuwa na kitu cha kusema, wapumbavu husema ili mradi waseme chochote”. Ni dhahiri kwamba Wapinzani hawana cha kuwaambia Watanzania kwa muda huu hivyo sio muda muafaka kwao kutaka kuzunguka nchi nzima kuwahadaa wananchi. Hata hivyo upinzani wanatakiwa kulishukuru sana jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa kwani kwa kufanya hivyo limewaondolea aibu kubwa ambayo wangeipata kwenye Ziara yao kwa kupuuzwa na wananchi.
Tunawataka
wabunge wa upinzani warejee Bungeni kuwawakilisha wananchi walio wachagua kwa
kuwatetea kwa hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa na sio vyama vyao pekee.
Vivyo
hivyo tunawaomba upinzani kubadilisha matumizi ya fedha walizokuwa wamepanga
kuzitumia kuzunguka nchi nzima, badala yake wazipeleke kwenye ununuzi wa
Madawati kwenye majimbo yao ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na uhaba wa
Madawati nchini.
Mwisho
japo sio kwa umuhimu UVCCM Mkoa wa Mbeya na Songwe tunawatakia waislam wote wa
Tanzania mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na tunawaomba watanzania
wote tuwape ushirikiano Ndugu zetu katika wakati huu muhimu kwa kutenda matendo
mema yampendezayo Mwenyezi Mungu.
MUNGU
IBARIKI MBEYA NA SONGWE, MUNGU MBARIKI MHE. DR. TULIA ACKSON MWANSASU MUNGU
IBARIKI TANZANIA.
Asanteni kwa kutusikiliza.
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa
na Amani L. Kajuna.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya & Songwe.
No comments:
Post a Comment