Wahitimu wa fani mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo kikuu cha TEKU baada ya kumalizika kwa Mahafali ya 9 yaliyofanyika juzi chuoni hapo |
Baadhi ya Wazazi jamaa na marafiki waliojumuika pamoja na Wahitimu wa Diploma ya Habari na mawasiliano kwa umma wakiwa katika picha ya pamoja |
Wahitimu wakiwa ukumbini wakifuatilia kwa makini matukio yanayoendelea |
Baadhi ya Wahitimu wa Fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya uuma wakiwa katika picha ya pamoja |
Wahitimu wa Fani ya Uandishi wa habari wakifurahia jambo baada ya kumaliza sherehe za mahafali, Wa kwanza kulia ni Godfrey Kahango kutoka gazeti la Mwananchi Mbeya. |
Baadhi ya Ndugu wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu Godfrey Kahango na Rogate Andrew |
Godfrey Kahango akiwa katika pozi |
Godfrey Kahango akifurahia kulishwa keki na dada zake akiwemo Amina Said kutoka Star Tv Mbeya (Kulia) |
Godfrey Kahango akilishwa keki na Venance Matinya ikiwa ni Ishara ya kumpongeza kwa kumaliza masomo yake ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma katika ngazi ya Diploma |
ILI
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa
ajira kwa vijana na wahitimu wa fanimbali mbali nchini, Uongozi wa Chuo kikuu
cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo jijini Mbeya umejipanga kuhakikisha
unaongeza kozi chuoni hapo.
Akitoa
taarifa ya kurugenzi ya Elimu Anuai ya Chuo Kikuu cha TEKU, Kaimu Mkurugenzi,
Simwaba Joseph alisema chuo kinatarajia kuongeza programu za uuguzi, ualimu wa
Sekondari na Msingi kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017 ili kusaidia vijana wengi kujinasua kutoka
katika wimbi la ukosefu wa ajira.
Kaimu Mkurugenzi huyo
alitoa taarifa hiyo juzi katika sherehe za Mahafali ya Tisa ya Chuo hicho
zilizofanyika katika Ukumbi wa mikutano uliopo Block T jijini Mbeya ambapo
wahitimu walitunukiwa Shahada katika fani mbali mbali ikiwemo Uandishi wa
habari na mawasiliano kwa umma.
Joseph
alisema katika Mahafali hayo jumla ya wanafunzi 191 waliajiandikisha lakini hadi
wanahitimu ni wanafunzi 157 watapewa
shahada kutokana na fani walizosoma, na wanafunzi 34 hawajaweza kuhitimu
mafunzo yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za wengine kushindwa kulipa
ada.
Awali
Akisoma risala ya wahitimu hao, Lwiza John, aliyesoma fani ya Uandishi wa
habari na mawasiliano kwa umma aliuomba uongozi wa chuo hicho kupunguza kiwango
cha ada kwa kuwa imekuwa ni mzigo kwao.
"Kiwango cha ada ni
kikwazo kwetu na tunaomba uongozi ulifikirie hili ili ada kwa mwanafunzi wa
astashahada ipungue kutoka Sh700,000 hadi 600,000 na stashahada ipungue kutoka
900,000 hadi 800,000," alisema Lwiza.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo, Profesa Tully Kasimoto aliiomba Serikali kuondoa utitiri wa kodi
wanazotozwa kwa shule na vyuo binafsi,hali
ambayo wamedai kuwa inadumaza utendaji kazi wao kwa kushindwa kuboresha huduma
hiyo muhimu kwa jamii.
Alisema vyuo binafsi
vinatozwa kodi nyingi tofauti na vyuo vya serikali hali inayowapa wakati mgumu
wamiliki hao na kupelekea wanafunzi kulalamikia ukubwa wa ada pasipokujua kuwa
sababu ni mlundikano wa kodi.
Alisema lengo la
wamiliki wa vyuo na shule binafsi ni kutoa huduma kwa vijana na siyo kufanya
biashara na kwamba wanashindwa kuboresha mazingira ya elimu kwa vijana kutokana
na fedha nyingi kutumika katika ulipaji wa kodi.
"Suala la kodi ni
changamoto kwetu kwani tunatoa kodi nyingi tofauti na vyuo vya serikali na hili
linadumaza utendaji kazi wetu kutokana na sisi tuna lengo la kutoa huduma kwa
vijana na siyo kwamba tunafanya biashara, "alisema Kasmoto.
Kuhusu udahili wa
wanafunzi wasiokuwa na sifa ya kujiunga na vyuo, Kasmoto alisema suala hilo
linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani wanaodahili wanafunzi hao wamekosa
uaminifu na hawana nia nzuri ya kukomboa vijana.
"Hivi sasa serikali
ndiyo inasimamia suala hilo la udahili wa mfumo wa pamoja na ili kuhakikisha
vyuo havidahili wanafunzi hewa ni vyema mfumo uchunguzwe upya na hata hivyo
mwanafunzi huyu kwa vyovyote vile atashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani
yake, "alisema.
No comments:
Post a Comment