Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya Isakwisa Mwambulukutu akisoma tamko la kumuunga mkono Rais Magufuli kwa utendaji wake. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya Isakwisa Mwambulukutu akisoma tamko la kumuunga mkono Rais Magufuli kwa utendaji wake kwa wandishi wa habari. |
Mmoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya akifuatilia kwa makini tamko la kumpongeza Rais Magufuli |
Baadhi ya Wazee wa CCM wakifuatilia tamko lililosomwa na mwenyekiti wao la kumpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake. |
WAZEE
wastaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jiji la Mbeya wamempongeza Rais wa awamu
ya Tano Dk.John Magufuli katika juhudi zake za utekelezaji mzuri wa ilani
ya uchaguzi mkuu wa 2015 na kuahidi kumuunga mkono.
Akisoma
tamko mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la
Mbeya, Isakwisa Mwambulukutu, alisema lengo la wazee kumpungeza ni juhudi zake
ambazo ni kuboresha maisha ya kila mtanzania kwa kuhimiza ufanyaji kazi kwa
bidii kwa kauli yake ya “hapa kazi tu”.
Alisema
Rais Magufuli katika uongozi wake amesimamia uwajibikaji na uimarishwaji wa
watumishi wa umma ambapo matokeo ya hivi sasa yameonesha mabadiliko kutoka
kufanya kazi kwa mazoea katika sekta za umma hadi kuwa kwenye mfumo ambao kila
mtu anaona serikali inawajibika.
Alisema
maeneo mengine aliyosimamia Dk. Magufuli ni pamoja na kupambana na rushwa,
ukwepaji kodi na ubadhilifu wa mali za umma kwa kutumbua majipu, kuboresha
huduma za jamii ili kuleta hali nafuu ya maisha ya watanzania kama huduma za
Hospitali na elimu bure kuanzia awali hadi sekondari .
Aliongeza
kuwa suala la kufufua na kuhimiza ujenzi wa viwanda jambo ambalo litachangia
ongezeko la vijana kupata ajira hivyo kupunguza uwezekano wa kukaa bila kufanya
kazi na kujiingiza kwenye vitendo viovu.
“Katika
sekta ya viwanda ni vema akatupia jicho katika viwanda ambavyo vimekufa jijini
Mbeya kama vile kilichokuwa cha kutengeneza sabuni (HISOAP), kutengeneza zana
za kilimo(ZZK), kiwanda cha nguo(Mbeya textile) na kiwanda cha Nyama cha
Tanganyika Peakers.
Wazee hao
mbali na kumpongeza Rais katika maeneo hayo pia walimuomba Dk. Magufuli
kuhakikisha anasimamia vema suala la matibabu bure kwa wazee kwani mbali na
uwepo wa utaratibu huo lakini huduma wapatayo hairidhishi.
Walisema
ili waweze kumudu matibabu kiurahisi ni vema Serikali ikawaingiza kwenye
mfumo wa Mfuko wa bima ya afya ya Tifa ili kuwarahisishia kuweza kupata
matibabu katika Hospitali zozote bila kutegemea sehemu moja ya Hospitali ya
Serikali.
Waliongeza
kuwa wanaomba pia Wazee wote ambao hawalipwi pensheni kwa vile hawakuwa
watumishi wa umma walipwe ili kuwapunguzia makali ya maisha pia kuwaboreshea
wale ambao wako kwenye mfumo kulingana na wakati.
No comments:
Post a Comment