|
Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali
– Richard Makungwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa NMB Executive
Network uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. NMB iliandaa mkutano
uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda
ya Nyanda za juu wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi
ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine, walipewa mafunzo na
kujadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na
wateja wake.
|
|
Afisa
Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu
ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network) Lightness Ndelwa
anayemiliki duka la lightness Fashions katika mkutano uliofanyika jijini Mbeya
mwishoni mwa wiki. NMB iliandaa mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na
wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda ya nyanda za juu na wenye mzunguko
wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi ya wateja 100 walihudhuria
ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya
kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja wake. Katikati ni Meneja wa NMB
Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.
|
|
Afisa
Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu
ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network membership)
Mfanyabiashara wa Simu jijini Mbeya –Esther Mbogela. NMB iliandaa mkutano
uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda
ya nyanda za juu na wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10.
Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana
jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja
wake. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.
|
|
Afisa
Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu
ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network membership)
Mfanyabiashara maarufu wa mbao jijini Mbeya - Bi Esther Mbilinyi katika hafla
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. NMB iliandaa mkutano
uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda
ya nyanda za juu na wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10.
Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana
jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja
wake. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.
|
NMB Executive Network (NEN) Ni mtandao wa wateja
wakubwa na wanaochipukia wenye mzunguko wa fedha kuanzia shilingi Bilioni 10
kwa mwaka. Tunawakaribisha pia wateja na wasio wateja wa NMB kwaajili ya
kuwaonyesha fursa na bidhaa za NMB.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini
Mbeya, Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali, Richard Makungwa alisema Mpango huu ulianza mwaka 2014 huku ukilenga miji
mikubwa 6 nchini yaani Dar es Salaam , Mwanza, Mbeya, Morogoro, Arusha and
Kilimanjaro.
Alisema Mpaka sasa, mtandao huu upo
kwenye mikoa mitano tu ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro.
Alisema
kwa Mkoa wa Kilimanjaro (Moshi), mtandao huu upo mbioni kuzinduliwa na utazinduliwa
sambamba na Kituo kipya cha biashara cha
NMB (New Business Center) ambapo mpaka
sasa, tuna washirika 286 wa mtandao wa NMB Executive Network.
Makungwa alisema Makusudi makubwa ya
kuanzisha mtandao huu ni kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya benki na
wateja wake na kuweka mahusiano yenye tija kwa pande zote mbili yaani kwa mteja
na kwa upande wa benki huku tukiangazia wateja wakubwa tu.
Alizitaja faida za mtandao huo kuwa ni pamoja na Uwezeshaji
kimaarifa (Elimu juu ya mipangilio ya Biashara, elimu ya kodi pamoja na
taratibu mbalimbali za serikali juu ya biashara).
Faida nyingine ni wateja kupata Fursa ya kukutana na uongozi wa juu wa
benki pamoja na menejimenti na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, Fursa ya
kukutana na wafanyabiashara mbalimbali
na kubadirishana mawazo,Fursa ya kutoa mapendekezo juu ya bidhaa za NMB, Fursa
ya kutoa mrejesho wa huduma za kibenki za NMB.
Alizitaja faida zingine kuwa ni Kupata upendeleo kwa
kupewa kadi maalumu za uanachama zinazokupa upendeleo wa huduma unapotembelea
matawi yetu nchi nzima,Kupata upendeleo wa bei ya kubadirisha fedha za kigeni.
No comments:
Post a Comment