Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati wa kliniki ya Michezo iliyofanyika uwanja wa Sokoine jijini |
Wachezaji waliohudhuria kliniki ya michezo wakijadiliana moja ya somo |
Wachezaji wakifuatilia somo la michezo |
Wachezaji wakiwa katika mazoezi ya vitendo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya |
VIJANA wametakiwa kucheza mpira
kama ajira ili kufikia malengo ya kucheza kombe la dunia na hatimaye kupata
nafasi ya kucheza soka la kulipwa.
Wito huo ulitolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa alipokuwa akitoa mafunzo ya Ulinzi na
Ushambuliaji kwa vijana yanayofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mafunzo ya siku tatu ya kliniki
ya michezo kwa ajili ya ulinzi na ushambuliaji yalifunguliwa na Mdau wa Michezo
nchini Ndele Mwaselela katika Uwanja wa
Sokoine Jijijini Mbeya yatakayodumu kwa siku tatu kuanzia Februari 12 hadi 14
mwaka huu.
Akifungua mafunzo hayo,Mwaselela
aliwataka vijana kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ili yaweze pia kuwapatia
ajira.
Ndele alisema kuwa Washiriki
wakizingatia mafunzo hayo ambayo ni adimu nchini yatawawezesha kwenda nje ya
nchi ili kupata mafunzo katika shule rafiki iliyopo Ujerumani.
Akifungua mafunzo hayo Mgeni
rasmi ametoa shilingi laki nane ili kufanikisha mafunzo hayo yanayogharimu
zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya chakula na vifaa vya kufundishia.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo
hayo Nyerembe Munasa alisema kuwa mafunzo hayo ya siku tatu yatawajengea uwezo wa mbinu stadi na ufundi ambao baadhi yao
wamenufaika kwa kwenda nje ya nchi kama Afrka Kusini na Brazil kwa mafunzo
zaidi.
Munasa ambaye ni Mmililiki wa
Kituo cha Elimu Mwendo(Human Kinetics Academy)alisema atatoa mafunzo hayo ya
siku tatu kwa vijana zaidi ya mia moja Jijini Mbeya wakizingatia vipaji vya Soka nchini na kuweza
kutoa wachezaji wa kimataifa.
Mmoja wa Washiriki wa mafunzo
hayo kutoka kituo cha Elimu Mwendo kwa niaba ya washiriki amemshukuru
Mwezeshaji wa mafunzo hayo na Mgeni rasmi kwa kupata mafunzo hayo ambayo
yatawasidia katika soka.
Kwa upande wake Katibu wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Harub Seleman amempongeza Mkufunzi wa semina
hiyo na kumuomba asikatishwe tamaa kwa mahudhurio hafifu ya washiriki na kwamba
waliotarajiwa kushiriki mafunzo ni zaidi ya 200 lakini waliohudhuria si zaidi
ya 30.
Mafunzo hayo yatamalizika
Februari 14 katika Uwanja wa Sokoine na kuwawezesha kumudu ulinzi na
ushambuliaji kisayansi hivyo kulifanya soka la Tanzania kuwa la kisasa.
No comments:
Post a Comment