Mratibu wa Taifa wa Shirika la Kimataifa la kuhudumia Viwanda, UNIDO. Deodat Bernard akitoa mada kwa Wahitimu wa Vyuo vikuu kuhusu Program ya kupambana na ajira kwa vijana |
Mwezeshaji wa Programu ya ajira kwa vijana Dk.Darlene Mutalemwa kutoka Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam akieleza umuhimu wa vijana kujiunga na mpango huo. |
Afisa maendeleo ya Biashara wa SIDO Mkoa wa Mbeya, Merina Mkuchu akisisitiza jambo kwa vijana waliojitokeza katika ukumbi wa Mkapa kuhusu mpango wa ajira(hawapo pichani) |
Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Wawezeshaji |
Baadhi ya Wajisiliamali wadogo na Kati wa Jiji la Mbeya wakielezwa juu ya umuhimu wa kuwapokea Vijana waliohitmu Vyuo Vikuu katika Biashara zao ili kubadilishana nao ujuzi |
SERIKALI ya Tanzania kwa
kushirikiana na Mashirika ya kimataifa imeandaa mpango wa jinsi ya kuwasaidia
vijana waliohitimu katika Vyuo vikuu ili wawe na uwezo wa kupata ajira bila
kutegemea kuajiriwa.
Akizungumza katika Mafunzo kwa
Vijana waliohitimu Vyuo vikuu kuanzia ngazi ya Diploma, Mratibu wa Taifa wa
Shirika la kimataifa la Maendeleo ya Viwanda(UNIDO), Deodat Bernard alisema Serikali
ilikuja na mpango huo ili kuona jinsi inavyoweza kutatua changamoto ya ajira
kwa vijana.
Alisema katika Mpango huo ambao
uliratibiwa na Shirika la UNIDO kwa kushirikiana na Shirika la
Kazi(ILO),shirika la Chakula (FAO) na UN Women ambao walichagua program ya
kuimarisha jinsi vijana wanavyoweza kupata ajira Program inayoendeshwa na Chuo
kikuu cha Mzumbe.
Alisema katika Program hiyo
vijana watakaochaguliwa wataweza kufanya kazi ya kujitolea na Wajasiliamali wa
kati na wadogo ili waweze kupata ujuzi kwa vitendo pamoja na kuwasaidia
wajasiliamali kuongeza na kuinua shughuli zao kupitia vijana waliosoma.
Kwa upande wao Wawezeshaji wa
Programu hiyo, Dk.Omary Swalehe na Dk.Darlene Mutalemwa kutoka Chuo kikuu
Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam walisema program hiyo kwa majaribio inawalenga
vijana 150 nchi nzima na kwamba tayari maelekezo yamefanyika katika ya Dar es
salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Dk. Swalehe alisema mpango huo
utaanza kutekelezwa Mwezi huu February hadi Juni Mwaka huu ambapo baada ya
kufanya tathmini na kubaini mafanikio kwa Wajasiliamali kunufaika ama Wahitimu
kuleta tija ndipo mikakati ya kuifanya iwe endelevu itafanyika.
Alisema Mpango huo
unaofadhiliwa na Kampuni ya Maendeleo la Sweden(SIDA) Wahitimu watapewa vyeti
baada ya miezi mine ya majaribio ambapo watakuwa wakijitolea kwa gharama zao na
kwamba vyeti hivyo vitakuwa na nembo ya Chuo kikuu Mzumbe na UNIDO ili
kumuongezea sifa atakapopata nafasi ya kuitwa kazini.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Biashara wa
SIDO, Merina Mkuchu mbali na kuipongeza UNIDO aliwasihi vijana watakaofuzu
kwenda kuzitumia taaluma zao kwa vitendo ili kujiimarisha na kujifunza zaidi
ikiwa ni pamoja na kumsaidia Mjasiliamali.
Alisema wanapoingia kwenye huo
mpango wasiwe na wasiwasi na taaluma na sifa za masomo waliopitia Vyuoni bali
kupitia Mjasiliamali anaweza kubadili mawazo na kuendelea na ujasiliamali ama
kuajiriwa na Mjasiliamali aliyekuwa akisaidiana nae kwenye kazi.
No comments:
Post a Comment