Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka NEC, Hamis Mkunga aliyemwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi akifungua mkutano na viongozi wa Asasi za Kiraia |
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro akielezea Changamoto alizoziona kwenye uchaguz wa Oktoba 2015 |
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mbeya, Costantino Mushi akifunga mkutano wa Tume na Viongozi wa Asasi za Kiraia |
Afisa Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya Vicent Msola akielezea mapungufu aliyoyabaini wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita |
Washiriki wakifuatilia mada na mijadala inayoendelea |
TUME ya Uchaguzi NEC imekutana
na viongozi wa Asasi za Kiraia na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri za
Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi kufanya tathmini ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba
2015.
Akizungumza katika kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya GR iliyopo Soweto Jijini Mbeya,
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka NEC, Hamis Mkunga
aliyemwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alisema lengo la kikao
hicho ni kufanya tathmini ya Uchaguzi mkuu uliopita.
Kwa upande wake washiriki wa
mkutano huo walisema Uchaguzi ulijawa na changamoto nyingi ambazo Tume inapaswa
kuzifanyia kazi mapema kabla ya uchaguzi mwingine kuitishwa.
Walisema Changamoto hizo ni
pamoja na kuimarisha daftari la wapiga kura kuanzia sasa kwa kuwaandikisha
vijana ambao kwa sasa umri umeshafika na vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi
ujao watakuwa wametimiza.
Lucy Mng’ong’o na Faustina
Valleri walisema mbali na elimu kwa mpiga kura zilizotolewa na Asasi za kiraia
bado kunachangamoto za wananchi kutojitokeza kupiga kura huku idadi kubwa ya
wanaoharibu kura pia kuwa kubwa.
Kwa upande wake Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,
Dk. Samwel Lazaro alisema Changamoto zinazoukumba uchaguzi zinatokana na maandalizi
na utekelezaji wake kuwa kama dharula.
Alisema suala la ucheleweshaji
wa vifaa, kutokutimia na majina ya mpiga kura kutokuwepo kwenye daftari ili
hali kitambulishi anacho bado ni changamoto inayojirudia kila uchaguzi hivyo ni
vema Tume ikaziamini Halmashauri kuhakiki vifaa vyote vinavyotakiwa kabla ya
kumkabidhi wakala.
No comments:
Post a Comment