Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini |
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya, Jaji Noel Chocha akielezea malengo ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo |
Baadhi ya Wanasheria na Mahakimu wa Mahakama za Mkoani Mbeya wakiwa katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini iliyozinduliwa kimkoa katika Stendi ya daladala Kabwe jijini Mbeya |
Baadhi ya wananchi wakifuatilia uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini yaliyofanyika katika kituo cha daladala jijini Mbeya |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro amezindua rasmi wiki ya sheria
nchini inayoadhimishwa kimkoa katika kituo cha daladala Kabwe jijini Mbeya.
Katika uzinduzi huo Kandoro
ametoa wito kwa wananchi kuwaepuka watu wanaojiita wanasheria wa mitaani(power
of attoney) kwani wanachelewesha na kupotosha upatikanaji wa haki kutokana na
kufanya kazi kwa njia ya utapeli.
Kandoro alisema wananchi
kupitia wiki hili wajitahidi kuhudhuria kupata mafunzo juu ya njia mbali mbali
za kupata haki badala ya kuwatumia matapeli wa mitaani wanaowadanganya na
kuwatapeli.
“Hawa wanaojiita power of
attoney tunapaswa kuwaepuka sana pia tulitumie wiki hii kujifunza njia sahihi
za kufuata kupata haki kwani hawa watu ni matapeli ndiyo wanatengeneza mianya
ya rushwa na kula fedha za mlala hoi kwa kutokujua haki na njia sahihi” alisema
Kandoro.
Aidha alitoa wito kwa Mawakili
wa kujitegemea kupunguza gharama za kuendeshea kesi ili kuwawezesha wananchi
wenyekipato cha chini kuweza kumudu kupata msaada wa kisheria kutoka kwa
mawakili.
Alisema kutokana na gharama za
mawakili kuwa kubwa ndiyo inayosababisha vishoka wa sheria kuibuka mitaani kwa
ajili ya kumpunguzia gharama mlalamikaji ili aweze kupata msaada kwa gharama
ndogo.
Alisema pia wanapaswa kufungua
matawi vijijini na sio kubaki mjini ili kuweza kufikia maeneo mengi kwa wakati
sahihi sambamba na kuwafikia wananchi wengi.
Awali akimkaribisha mkuu wa
Mkoa, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Jaji Noel Chocha alisema
katika siku tatu za maadhimisho ya wiki ya sheria itakayohitimishwa Februari 4,
mwaka huu itaenda sambamba na utoaji wa elimu juu ya maswala ya sheria kwa
wananchi.
Jaji Chocha alisema maadhimisho
hayo hayajawahi kufanyika kwa kutoa elimu kwa wananchi hivyo itakuwa endelevu
kila mwaka ambapo katika maadhimisho hayo elimu itatolewa na mawakili wa
Serikali, mawakili wa kujitegemea, Jeshi la Polisi, idara ya ardhi na migogoro
na ustawi wa jamii na dawati la jinsia.
Alisema maadhimisho hayo yenye
kauli mbiu ya Wajibu wa Mahakama na wadau katika utoaji wa haki itafanyika katika vituo viwili katika Jiji la
Mbeya ambavyo ni vituo vya mabasi vya Kabwe na Nanenane.
No comments:
Post a Comment