Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akitoa taarifa juu ya Safari ya Wanachama wa TAJATI Wilaya ya Chunya kwa Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya(hayupo pichani) |
WanaTAJATI walipata fursa ya kutembelea wagonjwa na kutoa msaada kidogo katika Wodi la Wazazi na Watoto, Pichani ni Ezekiel Kamanga mwanachama wa TAJATI akimpa pole mgonjwa katika wodi la wazazi |
WanaTAJATI pia walipata fursa ya kushiriki upandaji wa miti kuzunguka eneo la Hospitali ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa |
Mbali na kupanda miti pia walifanya usafi katika mazingira yanayoizunguka Hospitali ya Wilaya ya Chunya |
TAJATI wakishiriki ujenzi wa daraja kubwa lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Igangwe kata ya Mtanila Wilaya ya Chunya linaloviunganisha vitongoji vya Shauri Moyo na Mtukula |
Wakulima wa Igangwe amcos wakishirikiana na Wanachama wa TAJATI katika upandaji wa miti |
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe akikagua timu za mpira wa miguu kabla ya kuanza kwa mtanange katika kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar |
Mtunza Hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akimkabidhi zawadi nahodha wa timu ya msindi wa Kwanza katika mechi maalum ya kuenzi mapinduzi ya Zanzibar |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli akiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI). |
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya. |
BAADHI ya Wanachama wa
Chama cha Waandishi wa habari za Utalii
na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) walifanya ziara ya siku tatu katika Wilaya ya
Chunya na kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii na kihabari.
Waandishi hao walifanya ziara
hiyo jumatatu na kukamilisha jumatano ya wiki hili ambapo wakiwa Wilayani
Chunya walipokea taarifa ya hali ya utalii ya Wilaya ya Chunya na kushiki
shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Akizungumza katika majumuisho
ya Ziara hiyo iliyojumuisha waandishi 12, mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka
Mwakilili alisema katika ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio imepokelewa vizuri
na wananchi.
Alisema siku ya kwanza
waandishi waliweza kutembelea wagonjwa na kutoa zawadi kidogo ikiwemo sabuni za
kufulia na vinywaji aina ya Grandmalt kwa ajili ya kuongeza nguvu sambamba na
usafi wa mazingira ulioenda sambamba na uzinduzi wa kupanda miti ambapo miti
zaidi ya 50 ilipandwa kati ya 560 inayotarajiwa kupandwa na Hospitali hiyo.
Aliongeza kuwa siku ya pili
waandishi hao walishiriki katika ujenzi wa daraja la Mto Lupa katika Mto kijiji
cha Igangwe linalounganisha Kijiji hicho na Vitongoji wa Shauri Moyo na Mtukula
lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili.
Aliongeza kuwa baada ya
kushiriki ujenzi wa daraja hilo waandishi hao pia walijumuika na wakulima wa
Chama cha Msingi cha Igangwe Amcos katika zoezi la upandaji wa miti ambapo
zaidi ya miti laki moja ilipandwa ikiwa ni kutekeleza utunzaji wa mazingira na
kampeni ya kata mti panda miti.
Zoezi hilo la upandaji miti
limetokana na wakulima wa Tumbaku kutumia miti kwa kiasi kikubwa wakati wa
kuandaa zao la Tumbaku hadi mavuno jambo lililopelekea uongozi wa Amcos kuweka
sheria na kanuni kwa kila mkulima kuhakikisha anapanda miti 500 katika shamba
la Chama cha msingi na 25 shambani kwake.
Mwakilili alisema mbali na
kushiriki shughuli hizo pia waandishi walizungumza na wananchi kuhusu
changamoto zinazowakabili ambapo mambo mengi yalibainishwa ikiwemo ndoa za
utotoni, mimba mashuleni na upungufu wa wahudumu wa afya katika kituo cha Afya
Mtanila ambacho kina watumishi wanne tu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Sophia Kumbuli mbali na
kuwapongeza WanaTAJATI kwa ziara yao
pamoja na shughuli zingine za kimaendeleo na kijamii aliahidi kuyafanyia kazi
mapungufu yaliyobainishwa.
Kuhusu ndoa za utotoni
Mkurugenzi alisema atawasiliana na Kamati ya Ulinzi na uasalama ya Wilaya ili
kuanza utekelezaji wa kuwasaka wanaume wanaooa mabinti wadogo na kuwakatika
katika masomo yao.
Alisema suala la afya kutokuwa
na watumishi wa kutosha alisemahilo ni tatizo la Wilaya nzima ingawa Serikali
inatarajia kutangaza nafasi za kuajiri hivyo tatizo hilo linaweza kupungua kwa
kiasi Fulani.
“Niwapongeze kwa juhudi zenu na
ninawaahidi kuyafanyia kazi mambo yote mliyoyabaini mkiwa Wilayani Chunya
hususani suala la kuozesha watoto wadogo hili limenisikitisha mno na
sitalifumbia macho nitatoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
ili wahusika wasakwe mara moja huu ni ukatili wa kijinsia” alisisitiza
Mkurugenzi.
No comments:
Post a Comment