Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi Jiji la Mbeya akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya Mkurugenzi. |
Maafisa Habari wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Jacqueline Msuya na John Kilua wakifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wakijitambulisha. |
Afisa habari wa Jiji la Mbeya, John Kilua akiomba ushirikiano kwa waandishi wa habari Mbeya. |
Baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wakiwa katika mahojiano na maafisa Habari wa Jiji la Mbeya katika Mkutano wa kutambulishwa. |
OFISI ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani hapa imeajiri maafisa Habari ili
kurahisisha mawasiliano baina ya Mkurugenzi, Wananchi na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa
habari wa habari wakati wa utambulisho wa Maafisa hao, Mkuu wa Idara ya Utawala
na Utumishi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Erick Mapunda kwa niaba ya Mkurugenzi
alisema lengo ni kuwa daraja kati ya wananchi na waandishi wa habari katika
kuboresha utumishi wa umma.
Aliwatambulisha maafisa hao
kuwa ni Jacqueline Msuya na John Kilua ambao alisema mbali na kuwa daraja baina
ya waandishi na Ofisi ya Mkurugenzi pia itasaidia kuboresha mahusiano kati ya
watumishi wa Halmashauri na waandishi wa habari.
Kwa upande wao Maafisa hao
walisema kutokana na kuwepo kwa kitengo hicho Waandishi wa habari watapaswa
kufuata utaratibu endapo watakuwa na shida ya kupata ufafanuzi kutoka kwa
Mkurugenzi au mkuu wa idara.
Walisema ni vema Mwandishi wa
habari akapata kibali kutoka kwa Afisa habari ya kwenda kuonana na mhusika
endapo suala lake litakosa majibu kutoka katika ofisi ya Idara ya Habari ili
kuondoa usumbufu wa kurudishwa na kukosa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment