Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (TIA) akitoa risala katika Mahafali ya 13 ya Chuo hicho na Mahafali ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya. |
Mshehereshaji wa Mahafari ya 13 na ya 3 kufanyika katika kampasi ya Mbeya Charles Mwakipesile akiendelea na wajibu wake wa kuongoza sherehe katika viwanja vya Kampasi ya Mbeya |
Wahitimu wa TIA wa nyanja mbali mbali wakiwa kwenye muonekano tofauti wakati wakitunukiwa Vyeti vya uhitimu katika mahafali ya 13 yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya |
Wahitimu wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio katika mahafali ya 13 na ya 3 kufanyika katika Kampasi ya Mbeya |
Baadhi ya Wakufunzi na mgeni rasmi wakitoka katika eneo la sherehe baada ya kumalizika na kufungwa rasmi kwa mahafali ya 13 ya Chuo cha Uhasibu (TIA) |
Baadhi ya ndugu na jamaa wakifuatilia matukio mbali mbali wakati wa mahafali ya Wanachuo cha Uhasibu Kampasi ya Mbeya |
Kikundi cha Ngoma za asili kikitua burudani katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu kampasi ya Mbeya |
Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania
(TIA) tawi la Mbeya, wameiomba Serikali ya awamu ya tano kufuta kigezo cha kuwa
na uzoefu kazini ndipo uweze kuajiriwa kwenye taasisi na Serikalini ili
kuongeza wigo wa fursa za ajira.
Wahitimu hao 1,689 wa ngazi ya
cheti, stashahada na stashada ya uzamili walitoa rai hiyo kwenye mahali yao ya 13 na ya 3 kufanyika
Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya chuoni hapo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa aliyemwakilisha Waziri wa fedha.
Hata hivyo katika ahadi zake wakati
akiomba kura kwa watanzania, Rais Dk. John Magufuli aliwahakikishia
wananchi kwamba katika utawala wake atafute kigezo cha uzoefu na badala yake
mtu akitoka masomoni aombe na kupewa ajira kulingana na uwezo wake binafsi na
sio kuangalia kigezo za uzoefu.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu
wenzake, mhitimu Elizabeth Swai, alisema kwa muda wote wanaokuwepo chuoni
wanajifunza masomo kwa nadharia na vitendo hivyo wanapomaliza masomo yao
wanakuwa na uzoefu wa kutosha wa kufanya kazi.
“Hili suala kigezo cha uzoefu kazini
kiondolewe kabisa. ‘Hivi habari eti uwe na uzoefu kazini usiopungua miaka
mitatu’ inatukwamisha sana kwanza ajira zenyewe ni ngumu kupatikana halafu vikwazo
kibao. Hivyo tunaiomba Serikali ifute kabisa kigezo hiki kwani hapa chuoni
tumesoma kwa nadharia na vitendo,” alisema Swai.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Wizara ya Fedha, Profesa Isaya Jairo, alisema ni aibu kwa
taifa kuona vijana wanaomaliza masomo yao katika fani mbalimbali kuanza
kujihusisha kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kanuni za taaluma zao
ikiwamo rushwa, udanganyifu na wizi.
Alisema ‘Niwaombe sana, mnatoka hapa
mkiwa mmepikwa na mkapikika hivyo basi mkaoneshe na kuleta mabadiliko ya kweli
kwenye taasisi mtakazoajiriwa. Msiwe chanzo cha ubadhirifu na wizi, achaneni na
tama ya kutaka kutajirika kwa muda mfupi baada ya kuingia sekta fulani kwani
hicho sio ndicho mlichofundishwa hapa’.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya,
Nyerembe Mnasa aliwataka wahitimu hao kuonesha weledi wao na kuwa chachu ya
kuminya mianya yote ya badhirifu katika kazi zao za uhasibu na manunuzi na
kuwataka kuongeza nidhamu kwenye matumizi ya fedha za umma.
“Udhaifu na umasikini wa taifa lolote
lile upo kwenye kitengo cha usahibu na manunuzi, ambapo wahusika wasipokuwa
makini ujue taasisi hiyo lazima iyumbe tu. Hivyo basi nyinyi wahasibu na
maofisa wa ugavi na manunuzi hakikisheni manonesha nidhamu ya matumizi ya fedha
za umma,” alisema Nyerembe.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment