Baadhi ya ndugu katika kikao hicho
Sakata
la mke kuishi na wanaume wawili lachukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa
mume halali Rogers Halinga kuketi kikao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa
Mbarali Mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla
hawajafungua madai ya ugoni Mahakani na kudai fidia.
Kikao
hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa Baba mzazi wa Rogers Halinga mzee
Jason Halinga(95) Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki na
kumsikiza mke wa Rogers ili abaini ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni
wa nani baina ya Rogers au Biton Mwashilindi.
Mwanamke
huyo a(22) akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai kuwa
mtoto huyo ni wa Rogers kwa kuwa aliondoka baada ya kutokea mapishano na mumewe
akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na
Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa Biton ndipo alipoamua
kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki na cheti cha kuzaliwa jina la Biton.
Huku
ndugu wakihamaki kutokana na kauli hiyo na kwamba yeye atamke wazi mtoto ni wa
nani ndipo Juliana bila aibu kwa Baba Mkwe Mzee Jason Halinga alijibu kuwa
mtoto ni wa Biton Mwashilindi,ambapo alimkabidhi mtoto huyo mwishoni mwa mwezi
Octoba kwa hiari na wala hakuporwa kama alivyotoa taarifa Polisi.
Kauli
hiyo ya Juliana ililazimu kikao kupiga simu kwa mzazi wa Juliana anayeishi
Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto wao kwani ilidaiwa
kuwa Biton aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao na
kwamba Biton hakujua kuwa Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni
mwanafunzi wa VETA Mbeya na asimwambie kuwa yeye ni mwanandoa.
Baba
mzazi wa Juliana Hosea Mwalukasa alidai kuwa ni kweli Biton alifika kwake
lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga
hivyo kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa ugoni kwani
Juliana hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Kikao
hicho baada ya mvutano wa muda mrefu kiliamua kuwa endapo Biton anadai kuwa
mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la Zalida Biton(2) ni mtoto
wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi cha shilingi milioni kumi au
alipe n'gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto wake na kwamba Juliana bado ni mke
halali wa Rogers.
Kwa
upande wake Biton Mwashilindi alidai kuwa hayuko tayari kulipa pesa hizo na
kwamba yeye alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi Ocktoba 31 mwaka huu
kituo kikuu cha kat mbele ya maafisa wa Jeshi la Polisi na kwamba hana kesi ya
kujibu na kwamba anasubiri tu mtoto afikishe umri wa miaka saba ndipo amchuke.
Katika
suala hili baadhi ya wadau wamelalamikia Jeshi la Polisi kwa kuamua
masuala ya kisheria katika vituo vya Polisi badala ya mamlaka za kisheria zipo
kama mahakama kuliko uamuzi uliotolewa na hali hii husababisha baadhi ya
wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Wamedai
kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa vipimo vya DNA bado
hakujatutua mgogoro huu na kwamba bado suluhu katika ndoa hiyo hiyo itakuwa ni
kitendawiri kisicho na majibu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment