HIFADHI za taifa Tanzania (TANAPA)
imetakiwa kuainisha maeneo yote yenye vivutio vya utalii ambayo yanawezekekana
kuendelezwa na kuyatangaza kwa wananchi wote ili kila mwenye uwezo wa kuwekeza
apewe nafasi.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa
Maliasili na utalii, Lazaro Nyarandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya
habari katika mkutano wake uliofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika
mapumziko mafupi wakati akielekea mkoani Njombe kumuwakilisha Waziri Mkuu.
Nyarandu alisema Serikali inamikakati ya
kuhakikisha Watanzania ndiyo wanapewa vipaumbele vya kuwekeza katika sekta za
utalii kwa kujenga nyumba za kulala watalii, kujenga makambi, kujenga na
kuendeleza vivutio pamoja na kutembeza watalii.
Alisema jambo hilo litasaidia kuinua
sekta ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha watanzania kutembelea
hifadi mbali mbali na sio kusubiri wageni kutoka nje ya nchi.
Alisema ili kuongeza kasi ya watalii
kuingia nchini kila mwananchi anapaswa kujifunza kukarimu wageni hususani
wahudumu wa mahoteli ambao wamekuwa wakiwahudumia wageni kila wakati ili wawe
na moyo wa kurudi tena.
Kwa upande wa ujangili na mauaji ya
Tembo Waziri Nyarandu alisema hivi sasa kuna mafanikio makubwa kutoka na kila
Mwananchi kushiriki kulinda hifadhi na kuzuia majangili kuua wanyama ovyo kama
ilivyokuwa awali.
Alisema hivi sasa kuna ongezeko kubwa la
Tembo tofauti na kipindi cha nyuma baada ya serikali yake kuweka mikakati
kabambe ya kuwakabili wawindaji wote ikiwa ni pamoja na kuwafungia leseni
wawindaji waliokuwa wakiwinda kinyume cha sheria na kuhusika kwenye mauaji ya
Tembo.
Aliongeza kuwa hata mfumo wa kukabiliana
na ujenzi holela wa makazi na mahoteli ndani ya hifadhi za wanyama umechangia
kuongezeka kwa uzalishaji wa Tembo ambapo alisema kwa takwimu za mwaka jana
kuna ongezeko la tembo zaidi ya 70,000.
Alisema hivi sasa Serikali haina idadi
kamili ya tembo walipo nchini katika mbuga zote ambapo imeshaingia makubaliano
na nchi wahisani ili kufanya sense ya Tembo na Faru ili Serikali iwe na idadi
halisi ya wanyama hao nchini.
Alisema kazi hiyo imeshaanza kufanyika
ambapo Mwisho wa mwaka huu wanatarajia kupata majibu ambayo Serikali
itawangazia wananchi wote ili wajue idadi ya Tembo na Faru waliopo katika kila
hifadhi na mbuga za wanyama nchini.
“ Hivi sasa kusema ukweli kabisa mimi
Waziri hata nikiulizwa swali leo kuwa tuna tembo wangapi nchini sina majibu kwa
sababu hakuna mtu anayejua na wala hatujawahi kuhesabu jambo tunalitarajia
kulifanya sasa” alisema Waziri.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment