MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,
amewataka vijana kutokuchagua aina ya kazi bali kufanya kila jambo ili mradi
wanaisaidia serikali katika kupambana na upungufu wa ajira nchini.
Kandoro alisema Serikali inatengeneza
mazingira wezeshi kwa kila mtu kupata ajira na sio kumpa ajira kila mtu hivyo
kwa anayetoa ajira kwa mtanzania mwenzake anachangia kutekeleza malengo ya
serikalio ya kuhakikisha ajira zinapatikana.
Hayo aliyasema wakati akizindua magari
ya kisasa ya Kampuni ya Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mikao
ya Mbeya, Rukwa na Dar Es salaam ya Ndenjela Jet katika hafla iliyofanyika
Uyole kwenye ofisi ya kampuni hiyo jijini Mbeya.
Kandoro alizungumza hayo kufuatia
mmiliki wa mabasi hayo, Allan Mwaigaga kuajiri zaidi ya watu 50 huku
akizingatia haki sawa kwa kuwa na wanawake sawa na wanaume katika ofisi yake na
kuwa na dereva wa kike anayeendesha moja ya mabasi yake.
Alisema kuna umuhimu wa watu hususani
vijana wa kike kutokubagua aina ya kazi na ajira jambo litakalosaidia Serikali
kuondokana na wimbi la upungufu wa ajira kwa wananchi unaolikabili taifa.
Alisema Ndenjela ni mfano wa kuigwa kwa
kuwa ameweza kuajiri vijana bila kubagua jinsia ikiwa ni pamoja na kutekeleza
maazimio ya Raisi ya kuhakikisha na toa ajira sawa kwa wanawake na wanaume
yaani 50 kwa 50.
“ ndugu zangu tuige mfano wa huyu
mmiliki wa haya mabasi kutoa ajira kwa watanzania wenzetu kwani kazi ya
serikali sio kuajiri kila mtu bali ni kutengeneza mazingira wezeshi kama
alivyofanya Mwaigaga kwa kuajiri watanzania zaidi ya 50 bila kubagua” alisema
Kandoro.
Kwa upande wake mmiliki wa mabasi hayo,
Allani Mwaigaga, ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mwaji group workshop,
alisema amelazimika kubuni magari ya kisasa kulingana na mahitaji ya watanzania
yenye lengo kubwa la kyupunguza ajali nchini.
Alisema magari yake yataweza kuwa mfano
hapa nchini kwa kupungiuza ajali kwa kiwango kikubwa kutokana na kufungiwa
kifaa maalumu ambacho kitakuwa kikiyaongoza magari hayo pamoja na dereva
anayeendesha na kutoa taarifa kama atakiuka sheria za usalama barabarani.
Alisema magari hayo yamefungiwa mtandao
wa WIFI ambapo kila gari litakuwa likiongozwa na watu wanne akiwemo Dereva
hivyo watuwengine watakuwa wakibaki Mbeya katika chumba maalumu wakifuatilia
mwenendo wa gari kila hatua linapokuwa likisafiri.
Naye mtaalamu wa mitambo ya magari hayo,
Joshua Mshanga, alisema vifaa vilivyofungwa kwenye magari hayo vinasaidia
kupunguza ajali zinazotokana na ulevi, mwendokasi na kuyapita magari mengine
sehemu za hatari.
Alisema kifaa cha GPS kilichofungwa
kwenye magari hayo kinawezesha aliyekuwa kwenye chumba cha kuongozea magari
kujua gari lilipo, kama dereva anayeendesha ni mlevi, spidi ambayo gari
linatembea au dereva akienda tofauti na alikopangiwa ambapo kifaa hicho hutuma
taarifa haraka na kutoa hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa wakati huo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Ndnjela, or Allan Mwaigaga, tunaomba uwe mfano wa kuigwa kwa kuwa na usafiri wenye usalama na wa makini. Wamiliki wa magari wamtegemee Mungu sio kutegemea makabrasha mengine yanayoteketeza roho za watu pasipo kosa. Ukimtegemea Mungu biASHARA YAKO ITAKUWA IMARA SIKU ZOTE. TUNAOMBA USALAMA WA RAIA WETU
Safi sana. Huyu mzee mbunifu sana. Walianza naye biashara enzi hizo wote walishafilisika. Hii inajieleza kwanini yeye yupo kwenye game mpaka leo.
Post a Comment