Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 13, 2014

SIKU YA FIGO DUNIANI,WATU KIBAO WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA LEO

Kaimu kurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Daktari Omari Salehe  akiongozana na mgeni rasmi Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga kwenda kuangalia vifaa mbalimbali vya kupimia figo

Dkt  Octabenny Kassanga akitoa maelezo kwa meya wa jiji la Mbeya jinsi vifaa hivyo vinavyofanya kazi

 Daktari Onesmo Kisanga kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. katikati akimfafanulia jambo meya wa jiji Athanas Kapunga 






Wananchi mbali mbali wa Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika upimaji figo bure





Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha Hospitali ya Rufaa Mbeya kupata vifaa vya kupimia magonjwa ya figo.

Kauli hiyo ameitoa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya katika maadhimisho ya siku ya figo nchini ambapo wakazi wa Mbeya wamejitokeza kupima ili kujua Afya zao na maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Daktari Onesmo Kisanga kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kisanga ambaye ni Rais wa Madaktari wa figo nchini amesema hivi sasa kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa figo kila siku hiyo inatokana na wananchi wengi kutopima afya zao hali ambayo ingeweza kuzuia matatizo makubwa ambayo hupelekea gharama kubwa za upasuaji.

Aidha Daktari bingwa amesema pia uhaba wa Madktari wa fani hiyo unawafanya waliopo kupata msongamano mkubwa wa wagonjwa kutoka mikoani pia wengi kofahamu kuwa hivi sasa Serikali imesogeza huduma hiyo katika Hospitali za Rufaa ikiwemo Mbeya yenye madaktari watatu wa figo.

Kati ya Madaktari watatu wawili ni raia wa Cuba na mmoja ni Mzalendo anayefahamika kwa jina la Octabenny Kassanga ambaye amewataka wananchi wa Mbeya kufika Hospitali ili waweze kujua Afya zao na kupatiwa tiba sahihi na ushauri ili kudhibiti ongezeko la ugonjwa huo ambao ukicheleweshwa gharama zake ni kubwa ambazo na zaidi ya shilingi milioni ishirini.

Kaimu kurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Daktari Omari Salehe amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Hospitali ya Rufaa ili kuokoa gharama kwani wanazo mashine za kisasa pia mdaktari waliobobea katika fani ya magonjwa ya figo ambapo katika siku mbili wagonjwa watapatiwa huduma ya vipimo bure kuanzia Machi 12 hadi Machi 14 mwaka huu.

Na Mbeya yetu

No comments: