WANAWAKE WA MUST
WANAWAKE
wameshauri bunge maalumu linaloendelea na Mchakato wa katiba mpya
kuhakikisha wanaweka vipengele ambavyo vitamtambua na kumpa haki za Msingi
Mwanamke.
Aidha
imeelezwa kuwa katika Katiba hiyo pia ikemee mila potofu zinazomdhalilisha
mwanamke kama vile ukeketaji na ndoa za umri mdogo pamoja na unyanyasaji wa
kijinsia hususani wajane kupokonywa haki za kurithi na kusimamia miradi
inayoachwa na mumewe.
Hayo
yalitolewa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya(CCM), Dk. Mary Mwanjelwa
wakati akizungumza na wanawake katika kilele cha Siku ya Mwanamke duniani,
ambapo alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe zilizoandaliwa na Wanawake wa Jiji la
Mbeya zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe jijini
hapa.
Dk.
Mwanjelwa alisema endapo haki za Mwanamke zikatambuliwa kikatiba itakuwa njia
rahisi kusimamia na kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka na kwenda
kinyume.
Aliongeza
kuwa Siku ya Wanawake duniani ilitokana na mfumo dume uliosababisha wanawake
kudai haki zao bila mafanikio hivyo kupelekea kuwepo kwa siku maalumu ya
kukumbushana mambo yanayopaswa kukemewa.
Aidha
aliwataka wanawake kuacha kubweteka kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya
kuwatetea bali wafanye kazi kwa bidii ili kutoa nafasi ya kuepuka kuwa ombaomba
na kunyanyaswa na waume zao.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment