|
Wachungaji na baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya kumsindikiza Pacha wa pili (Anania)aliyefariki dunia kati ya mapacha wanne waliozaliwa na Aida Nakawala mkazi wa Kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya |
|
Msafara wa kuelekea katika makaburi ya kijiji tayari kwa mazishi ya Pacha wa Pili kati ya mapacha wanne aliyefariki kwa ugonjwa wa Nimonia |
|
Mchungaji wa kanisa la Africa Mission Church akiendelea na ibada ya mazishi makaburini tayari kwa safari ya mwisho ya mtoto Anania |
|
Mwili wa Marehemu ukishushwa kaburini |
|
Katikati ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za juu kusini, Ahmed Issah pamoja na wafanyakazi wake wakiwa makaburini kumsindikiza marehemu ambapo pia Mamlaka hiyo ndiyo iliyosafirisha mwili wa marehemu kutoka Hospitali ya Wazazi Meta walikokuwa wakipatiwa matibabu. |
|
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za juu kusini, Ahmed Issah, (wa kwanza kushoto)akisaidia kufukia kaburi la marehemu pia Mamlaka hiyo ndiyo iliyosafirisha mwili wa marehemu kutoka Hospitali ya Wazazi Meta walikokuwa wakipatiwa matibabu. |
|
Baba wa Marehemu Weston akiwa amekaa kwa unyonge huku akifuatilia mazishi ya mwanae |
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za juu kusini, Ahmed Issah akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mamlaka ya hali ya hewa kutokana na kuguswa na msiba huo
|
Shomi Mtaki ambaye ni mwandishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo kutoka Wilaya za Momba na Mbozi akizungumza jambo kwa niaba ya waandishi wa habari ambapo alisema jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kufunga na kuomba kwa ajili ya maisha yao kutokana na kufanya kazi katika mazingira magumu. |
Shomi Mtaki akitoa rambi rambi yake kwa familia ya marehemu
|
Haya ni makaburi mawili waliyozikwa mapacha wawili Alinikumbu ( wa kwanza kuzaliwa) na Anania( wa tatu kuzaliwa) waliofariki dunia kwa siku tofauti kutokana na ugonjwa wa Nimonia uliosababishwa na hali ya Maisha duni ya kijijini kwao Chiwanda yanayowakabili wakazi wa huko.
WANANCHI
na wakazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya wametoa Pongezi
kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye makao makuu
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe(SIA) uliopo Mkoani Mbeya
kwa kufanikisha mazishi ya Mtoto mmoja kati ya mapacha wawili waliofariki
dunia kwa ugonjwa wa Nimonia.
Pongezi
hizo zimetokana na mamlaka hiyo kujitolea kusafirisha Mwili wa Marehemu kutoka
Hospitali ya Wazazi Meta walikokuwa wakipatiwa matibabu hadi Kijijini Kwao
Chiwanda Wilayani Momba.
Mbali
na usafiri huo pia msafara wa kuelekea kijijini kwa mazishi pia uliongozwa na
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda, Ahmed Issah akiongozana na wafanyakazi
watatu.
Akizungumza
kwa niaba ya familia Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mpumpi katika kijiji cha
Chiwanda,Winston Mtali alisema ni heshima kubwa iliyooneshwa na meneja huyo kwa
kuthamini msiba wa mtoto mdogo na kujitolea kugharamia usafiri na shughuli zote
kwa ujumla.
Alisema
mara nyingi shughuli za misiba kama hiyo huratibiwa na wananchi kwa ushirikiano
na serikali ya kijiji lakini katika mazishi ya Mapacha hao hali imekuwa tofauti
kutokana na uwepo wa misaada kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Nyanda
za juu kusini.
Aliongeza
kuwa viongozi wote wanapaswa kuonesha moyo wa kujitoa kwa watu wa hali ya chini
kama alivyofanya Meneja huyo pamoja na wafanyakazi wake kwa kuamua kutoa
usafiri na kushuhudia mazishi.
Kwa
upande wake Meneja huyo, Ahmed Issah alisema anayepaswa kushukuriwa zaidi ni
vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa za mara kwa mara
zinazohusiana na watoto hao tangu kuzaliwa hadi sasa na hawakuweza kukata tama.
Alisema
hata watu wanaotoa misaada ni kutokana na kupata taarifa zenye uhakika kutoka
kwa waandishi wa habari ambazo zimesaidia watu wengi kujua hususani wanaoishi
nchi za nje.
Alisema
hivi sasa watu hawahangaiki upataji wa taarifa juu ya jambo lolote isipokuwa
kwa kuingia katika mtandao wa Mbeya yetu Blog ambako hupata kila tukio linapotokea
kwa uhakika zaidi.
Akishukuru
kwa niaba ya Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mazishi ya mtoto huyo,
Shomi Mtaki ambaye ni mwandishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo kutoka Wilaya
za Momba na Mbozi alisema jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya
habari ikiwa ni pamoja na kufunga na kuomba kwa ajili ya maisha yao kutokana na
kufanya kazi katika mazingira magumu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment