Picha ya pamoja
KAMPUNI ya ALAF LIMITED inayozalisha
bidhaa mbali mbali za ujenzi kwa kutumia Vyuma, imekutana na wadau wa sekta ya
ujenzi hususani Makandarasi na mawakala wa vifaa vya ujenzi ili kutambulisha
bidhaa mpya pamoja na kupokea maoni juu ya uboreshaji wa bidhaa hizo.
Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa Hoteli ya GR City iliyopo Soweto Jijini Mbeya, ambapo uongozi
wa Kampuni ya ALAF uliwaambia wadau hao juu ya bidhaa wanazozalisha kuwa ni
Mabati maarufu kwa simba dumu ambayo wadau hao walielezwa namna ya kutofautisha
na mabati feki yanayotolewa na watu wengine.
Meneja wa tawi la ALAF Mkoani Mbeya,
Grayson Mwakasege, alisema lengo la mkutano huo ni kushirikisha wadau kuhusu
bidhaa zao mpya ili wajue namna ya kuzitumia na siyo kukutana nazo sokoni bila
taarifa yoyote.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na
Scafolding, Ultra-span (vyuma vya makenchi) na bati za rangi mbali mbali kutoka
Afrika Kusini ambapo washiriki wa Mkutano huo waliweza kutoa changamoto
wanazokutana nazo wakati wa matumizi ya bidhaa hizo.
Wadau hao walisema changamoto kubwa ni
bei ya bidhaa tofauti na vifaa vingine jambo ambalo lilibainika kuwa ni
kutokana na malighafi wanazotengenezea yaani Chuma kutolewa nchini Japan na
kusafirishwa hadi Dar Es Salaam ambako kipo kiwanda.
Kutokana na changamoto hiyo wadau hao
waliishauri kampuni ya Alaf kuchangamkia madini yaliyogunduliwa Mchuchuma ili
kupunguza gharama kwa wananchi kwa kuwa malighafi ya chuma itakuwa ikichimbwa
hapa hapa nchini.
Mwakasege aliwashauri wananchi na
watumiaji wa bidhaa zao kununua kutoka kwa mawakala waliowateua ili kuepuka
kununua bidhaa feki ambao ni Suju Hardware, TAFISA, Machemba na Ballus.
Aliongeza kuwa pia kampuni yao imeanza
kuzalisha Ultra- Span ( vyuma vya kuezekea) badala ya matumizi ya mbao kwa madai
kuwa itasaidia utunzaji wa mazingira kwa kutokata miti ovyo na kuimarisha
nyumba zao kutokana na majanga ya moto.
Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na
kampuni hiyo ni Bati, Tiles, Pipes, Contena(moveble house) na mirunda ya Chuma
badala ya kutumia miti.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Ssana ALAF Mbeya kwa kutoa taarifa kwa wateja wenu hongera pia kwa meneja wa tawi
Ssana ALAF Mbeya kwa kutoa taarifa kwa wateja wenu hongera pia kwa meneja wa tawi
Post a Comment