Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, September 5, 2013

WAKULIMA WAHIMIZWA KUTUMIA MBEGU ZILIZOFANYIWA UTAFITI WA KITAALAMU.

 Bwana Shamba wa Kampuni ya kuzalisha mbegu ya Highlands Seeds Growers, Idd Kapteni kutoka Chuo cha utafiti wa Kilimo Uyole Mbeya akielezea utumia wa mbegu bora kwa wakulima
Wakala mkuu wa Mbegu za Mahindi kutoka kampuni ya Highlands Seeds Growers anayesambaza Wilaya ya Makete, Tito Tweve amesema Mawakala wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu ya kumfikishia mkulima mbegu pale walipo.

Wakulima wakiwa katika mafunzo ya Mbegu bora





Baadhi ya wakulima wakiuliza maswali juu ya mbegu bora kwenye mafunzo hayo



Mratibu wa mafunzo kwa wakulima,Award Mtandilah amesema wakulima wanamwitikio mkubwa wa kutumia mbegu bora ambapo wengi wao wanatoka sehemu za mbali ambazo ni Vijijini


Wakulima wakipokea Mbegu




Wakulima nchini wameaswa kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti wa kitaalamu ili kuepuka kutumia mbegu feki zinazokwamisha juhudi za kufikia maisha bora.

Hayo yameelezwa  na Bwana Shamba wa Kampuni ya kuzalisha mbegu ya Highlands Seeds Growers, Idd Kapteni kutoka Chuo cha utafiti wa Kilimo Uyole kilichopo Mkoani Mbeya, wakati wa mafunzo ya matumizi bora ya mbegu za kisasa kwa Wakulima wa Mahindi wa Vijiji 12 vya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Kapteni amesema Wakulima wamekuwa wakilalamikia mbegu kutokuota vizuri mashambani kwao licha ya kununua mbegu bora kama Serikali inavyoagiza pamoja na kufuata kanuni za Kilimo kutokana na mawakala kutowaelekeza juu ya matumizi bora ya mbegu za kisasa.

Amesema ili kuondoa umaskini wa Mtanzania na Mkulima kulima kilimo chenye tija ni pamoja na matumizi ya mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na Taasisi ya Serikali na kuthibitishwa pamoja na kukaguliwa kwa kumuongezea kipato.

Akizungumzia mbegu bora amesema ni pamoja na UH 6303 na UH615 kutoka kampuni ya Highland Seeds ambazo zimefanyiwa utafiti kwa ajili ya kumudu mazingira ya Tanzania ambazo zinahimili magonjwa na hale ya Hewa iliyopo Nchini.

Amesema Mbegu hizo baada ya kufanyiwa utafiti huzalishwa na taasisi za Serikali ambazo ni Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Jeshi la Magereza kabla ya kumfikia Mkulima ili kujiridhisha na matokeo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Kilimo wa Wilaya ya Makete, Beda Kusenge, amesema Mkulima anapowaza kuzalisha kitu mbegu ni suala la msingi na la kwanza kuzingatiwa hivyo suala la matumizi ya Mbegu bora ni agizo la Serikali linapaswa  kuungwa mkono na kila mkulima ili kuendeleza dhana ya kilimo kwanza kwa vitendo.

Amesema katika uzalishaji Mbegu ina asilimia 30 ukiacha mbolea, madawa na gharama za utayarishaji wa Shamba, na kuongeza kuwa baada ya kuzingatia hilo Mkulima atarajie mavuno kuanzia asilia 30 bila kipingamizi cha aina yoyote.

Naye Wakala mkuu wa Mbegu za Mahindi kutoka kampuni ya Highlands Seeds Growers anayesambaza Wilaya ya Makete, Tito Tweve amesema Mawakala wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu ya kumfikishia mkulima mbegu pale walipo.

Amesema kutokana na umbali wa maeneo na miundombinu mibovu ya barabara hulazimika kuongeza bei ya Mbolea na Mbegu hali inayosababisha Mkulima kushindwa kumudu kununua Mbegu bora na hatimaye kulazimika kutumia zisizofanyiwa utafiti.

Ameongeza kuwa pia baadhi ya watu wamekuwa siyo waaminifu kwa maisha ya Watanzania kwa kuchakachua Mbegu na kuwauzia Wananchi na kusahau kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kumnyonya Mkulima asuyekuwa na hatia.

Aidha baadhi ya wakulima waliohudhuria mafunzo hayo wametoa wito kwa Serikali kuwabana wanaochakachua mbegu na kuziuza kwa kile walichodai kuwa wengi wao hawajui kusoma wala kugundua ubora wa mbegu na kuishia kushangaa zikishindwa kuota mashambani.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakulima watatu watatu kutoka Vijiji  12 vya Halmashauri ya Wilaya ya Makete pamoja na Mabibi na Mabwana Shamba wao pia walipatiwa mafunzo namna ya kufuata kanuni bora za upandaji wa mahindi sambamba na kugawiwa kilo mbili mbili za Mbegu za mahindi aina ya UH 6303 kwa ajili ya mfano kwa kila Mkulima aliyekuwepo.

Mratibu wa mafunzo kwa wakulima,Award Mtandilah amesema wakulima wanamwitikio mkubwa wa kutumia mbegu bora ambapo wengi wao wanatoka sehemu za mbali ambazo ni Vijiji vya Isapulano, Ivirikinge,Luvulunge, Ivalalila, Iwawa, Nduramo, Maleutsi,Kisinga, Ugabwa, Hevelo, Mago, Lupalilo na Ludihani.

Na Mbeya yetu

No comments: