Hakika hali ya amani imerejea tena sasa nifuraha tu
Hatimaye mgogoro baina ya wanakijiji cha IGUNDU Kata ya
SANGAMBI wilaya ya CHUNYA Mkoani
MBEYA na jamii ya WAFUGAJI umemalizika baada ya serikali wilayani humo
kuzikutanisha pande hizo na kuondoa tofauti zao.
Mgogoro huo uliodumu kwa wiki moja kufuatia baadhi ya vijana
wa kijiji hicho kumuua mfugaji aliyefahamika kwa jina la SAID PETRO kwa kipigo
kutokana na vijana hao kumtaka awape pesa naye kushindwa kutekeleza takwa lao
ndipo walianza kumpiga.
Kabla ya kupatanishwa wafugaji hao walikutana faragha kutoa
msimamo wao juu ya vitendo vilivyokithiri kutoka kwa wanakijiji cha IGUNDU
wakidai hilo ni tukio la tano kutokea na serikali ya kijiji haijachukua hatua
yoyote kukomesha vitendo hivyo.
Baada ya mjadala mrefu wafugaji walikubali kusogea meza ya
mazungumzo yaliyoongozwa na Afisa Tawala Wilaya ya CHUNYA AMIMU MWANDELILE
ambaye alilaani vikali kitendo kilichofanya na vijana hao kwani kitendo hicho
hakikubaliki na jamii kwani kinaondoa utu wa Mtanzania.
AMIMU amesema vitendo vya uhalifu kijijini hapo vinachangiwa
na unywaji wa pombe kupita kiasi na utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo vijana
wanatafuta njia ya mkato kutafuta pesa ikiwemo kucheza kamali badala ya kufanya
kazi.
Aidha amesema kuwa serikali haitafumbia macho vitendo hivyo
atahakikisha wale wote waliohusika na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria hivyo anayevunja
sheria hatavumiliwa kabisa.
Kwa upande wake AMIMU alichukua fursa hiyo kuwapongeza
wafugaji hao kwa moyo wa uvumilivu kwa kutolipa kisasi pamoja na vitendo vya
kikatili walivyofanyiwa wafugaji hao zaidi ya mara tano hata kupelekea wengine
kujeruhiwa na wengine kuuawa.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mweyekiti wa kijiji cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI alipatanishwa
na Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT ambao walipatanishwa na Afisa Tawala
Wa Wilaya ambapo pande hizo ziliahidi kukomesha vitendo hivyo na kwamba
wananchi wa IGUNDU waondoe hofu wao kama wafugaji hawatalipiza kisasi na
waendelee na shughuli za uzalishaji mali,
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment