Viongozi wa chaneta wakiongea na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Chama cha Netboli Taifa(CHANETA)
Annah Kibira anawaomba wapenzi wa mpira huo Mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa wingi
katika uwanja wa Sokoine kwa sherehe za kufunga ligi hiyo.
Kibira amesema ligi hiyo itahitimishwa kwa
michezi miwili ambayo ni kati ya Hamambe dhidi ya Jeshi Staa na mchezo mwingine
kati ya Filbert Bayi dhidi ya JKT Mweni.
Amesema katika michezo hiyo mgeni rasmi ambaye
anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
atashuhudia michezo hiyo kwa kuzikakugua timu hizo kabla ya kutoa zawadi kwa
washindi na kufunga.
Hata hivyo Kibira ametoa wito kwa wadau wa
michezo nchini kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili kuwa na mvuto kama michezo
mingine ili kuzifanya timu shiriki kuwa nyingi.
Kibira amesema kukosekana kwa wafadhili wa Ligi
za Netboli kumechangia timu kupungua katika Ligi daraja la Kwanza mwaka huu
ambapo kwa kawaida zilitakiwa kuwa na timu 20 lakini hadi ligi inafunguliwa
Agosti 24, Mwaka huu jumla ya timu 12 zilijitokeza na kushiriki ligi hiyo
itakayohitimishwa Septemba Mosi, Mwaka huu.
Alisema kutokana na kushiriki kwa timu chache
jumla ya michezo 66 ikakuwa imefanyika kufikia kesho kwa amani, Upendo na
Mshikamano ukihusisha timu 12 na kuongeza kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Chaneta
timu nane ambazo zilishindwa kushiriki zinatakiwa kushuka daraja hivyo hatima
yao Kamati tendaji itaamua.
Akizungumzia kilele cha kuhitimisha Ligi hiyo
Mwenyekiti wa Chaneta Mkoa wa Mbeya, Mary Mng’ong’o amesema Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Philipo Mulugo ambaye
atashuhudia michezo miwili na kugawa zawadi kwa washindi.
Mng’ong’o amesema undeshaji wa ligi hiyo
umekutana na changamoto nyingi lakini kubwa kabisa ni ukosefu wa fedha
uliotokana na uchangiaji duni wa wadau hali iliyopelekea timu kujigharamia
zenyewe.
Aidha ametaja msimamo wa ligi hiyo kuwa
inaongozwa na timu ya JKT Mbweni yenye alama 20 sambamba na timu ya Filbert
Bayi yenye alama 20 lakini ikiwa na magoli machache dhidi ya JKT Mbweni.
Timu ya Magereza Morogoro inashika nafasi ya
tatu ikiwa na alama 17 ikifuatiwa na Jeshi Staa yenye alama 15 na timu mwenyeji
ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya (HAMAMBE) ikishika nafasi ya tano kwa alama 13
huku timu ya Polisi Mbeya ikifunga mkia kwa alama 2 sambamba na CMTU kutoka Dar
Es Salaam ikiwa haina alama hata moja.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment