Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, August 22, 2013

Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN Ametoa vyeti kwa madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda zaidi ya 151 wa Igurusi Wilaya ya Mbarali.

Madereva Bodaboda wakijipanga tayari kwa kwenda kupokea vyeti vyao

Madereva Bodaboda wakiandamana kuelekea kupokea vyeti vyao toka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya


Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN akiongea na madereva Bodaboda kabla ya kuwakabidhi vyeti vyao
Madereva  walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa mafunzo ya alama za usalama barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya.


Picha ya pamoja




Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN Ametoa vyeti kwa madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda zaidi ya 151 wa Igurusi Wilaya ya Mbarali.

Madereva hao walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa mafunzo ya alama za usalama barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya.

Mbali ya kukabidhiwa vyeti pia Madereva hao walipatiwa leseni za udereva ambapo Diwani Athumani aliwataka madereva hao kuwa makini barabarani na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Aidha Kamanda Diwani aliwashukuru madereva wa Bodaboda kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa kufichua vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya ambapo wamekuwa wakitoa taarifa za siri na kupunguza uhalifu mkoani Mbeya.

Hata hivyo Diwani alitumia fursa hiyo kuwataka madereva kuwa makini kwani kwa kipindi cha miezi sita madereva 38 wa bodaboda wamefariki mkoani Mbeya na kusikitishwa na wingi wa ajali hizo za pikipiki kwani wengi wao ni vijana na ni nguvu kazi ya Taifa. 

Na Mbeya yetu

No comments: