Mkuu wa wilaya ya Chunya
Mheshimiwa Deodatus Kinawiro.
WAFANYABIASHARA wanaofanya biashara
za ununuzi wa mazao wilayani Chunya Mkoani Mbeya wamepigwa marufuku kununua zao
la ufuta bila kufuata taratibu za halimashauri hiyo.
Marufuku hiyo imetolewa juzi na Mkuu
wa wilaya hiyo Deodatus Kinawiro katika kikao cha baraza la madiwani.
Alisema kwa muda mrefu sasa wakulima wengi wa zao la ufuta katika wilaya hiyo
wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udanganyifu na wafanyabiasha hao kwa kufanya
ununuzi wa zao hilo kwa bei isiyo halali.
''Wafanyabiashara hao wanawaraghai
wakulima hao kwa kununua zao hilo bila kufuata taratibu za upimaji badala
yake wamekuwa wakitumia ndoo hali inayo fanya mkulima huyo kuendelea kuumizwa''
alisema Mkuu wa wilaya huyo.
Amesema serikali haipigi marufuku
ununuzi huo ili kumumiza mkulima bali inafanya hivyo ili kuinua pato la mkulima
kwa kuhakikisha anapata bei nzuri inayo mnufaisha.
Sanjari na hayo amepiga marufuku wafanyabiashara
kuwakopesha wakulima fedha kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kilimo.
|
No comments:
Post a Comment