Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 8, 2011

MCHINA AMWAGA MACHOZI BAADA YA KUKUTANA NA WASTAAFU WENZIE WALIOFANYA KAZI PAMOJA RELI YA TAZARA

MWENYEKITI wa Shirika la Ushirikiano wa Tanzania na nchi ya China SINOTA Friendship Association Bw. Jiang Jing  Ying leo asubuhi alishindwa kuvumilia na kujikuta akimwaga machozi baada ya kukutana na wastaafu wenzie waliofanyakazi pamoja Reli ya TAZARA miaka zaidi ya 40 iliyopita
Bw. Jing alikutana na wastaafu hao wa TAZARA na kuona hali zao za maisha ambapo mara baada ya kumaliza kusalimiana nao alianza kumwaga machozi akikumbuka namna ambavyo aliishi nao miaka hiyo huku wakiwa katika hali mbaya ya maisha tofauti na jinsi yalivyo maisha yake nchini China.
 Alisema kuwa ushirikiano uliodumishwa na marais wastaafu wa Tanzania Hayati Mwalimu Nyerere wa Tanzania na Hayati Mao Tse Tung wa China unapaswa kuendelezwa kwa kudumisha rasilimali zilizoachwa ikiwemo reli ya TAZARA ambayo inapaswa kutunzwa.
Bw. Ying ambaye pia ni Mkurugenzi wa makampuni kadhaa nchini China anasema kuwa hakutegemea kuwaona watu aliofanya nao kazi wakiwa katika hali duni ya maisha huku wengine wakiwa wamezeeka wakionekana wakishindwa kuendesha maisha yao kutokana na hali ngumu ya uchumi waliyonayo.
Alisema kuwa reli ya TAZARA imechakaa hali ambayo inaweza kusababisha kuibuka kwa ajali jambo ambalo linaweza kugharimu maisha ya watu, hivyo alishauri kuwepo na mikakati mbadala ya kuirejesha reli ya TAZARA katika hadhi yake kama ilivyokuwa miaka ya sabini.

Bw. Ying anakumbuka alivyofanya kazi kuanzia Kurasini Jijini Dar es salaam kati ya mwaka 1969 na baadaye Kisarawe kisha alihamia Mbeya na Mbozi hadi Tunduma ambako,amepanga kufanya ziara ya kuitembelea reli hiyo kuanzia Tunduma hadi Dar es salaam ambako amepanga kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili amweleze mambo muhimu juu ya uboreshaji wa reli TAZARA.

8 comments:

Mbele said...

Tanzania haina uongozi thabiti bali ubabaishaji. Matokeo yake ni kuwa tuna hela za kuwalipa Dowans na pia za watu kujichotea watakavyo, kama vile EPA.

Vile vile, tuna hela zisizo kifani za kununulia magari ya fahari kwa hao wanaotwa viongozi, kama lile gari alilolikataa Waziri Mkuu Pinda, lakini hakuna aliyepitisha uamuzi kuwa tusinunue tena magari ya aina hiyo. Vile vile, tuna rasilimali tele, kama vile madini, ambazo zinaporwa muda wote na wale ambao wanaitwa wawekezaji.

Nchi tajiri kama Tanzania ingeweza kuitunza hii reli vizuri iwapo ingekuwa na uongozi thabiti. Tatizo ni ubabaishaji na ufisadi.

Wakati huyu m-China anatokwa machozi, mafisadi wa Tanzania wanaendelea kukamua.

mbuso.kihara said...

Professor Mbele, inasikitisha sana kwa mtu mwenye uzalendo, ila viongozi wetu wamepoteza uzalendo na sasa ni ubinafsi hakuna anayetaka kuacha jina katika kuboresha maendeleo bali jina kati ya wale mafisadi.

Anonymous said...

Hali ya reli ya tazala inatisha ninaitumia kuanzia nianze kidatu cha kwanza mpaka sasa nipo chuo kikuu, tren linanuka,halina ratiba kamili,tulisha wai simama polini tukielekea makambako masaa tisa bila ya chakula tatizo tren liliisha mafuta nyinyi chukua chako mapema mnatutesa sisi walipa kodi wa mlimba, mngeta,chita,uchindile, hivi ni vijiji baadhi ambavyo watu wake wengine hata rami hawaijui tegemeo lao kubwa ni hii reli ya uhuru TAZARA mumuogope MUNGU AMEN.

Anonymous said...

Hali za watanzania daima zitazidi kuwa mbaya kwani wanaotuongoza daima ni wasio wazalendo na kujali..... Wataalamu na wafanyakazi pamoja na wananchi hawapewi kipaumbele.. Angalia hao wazeee duuuh.... Ndio maana madaktari wanagoma bkoz unaitumikia Tanzania lakini utaishia umaskini wa kutupwa kama hao wazee wetu..
UZALENDO KWA VIONGOZI SI MZURI

Unknown said...

Kwa kweli inasikitisha sana,ndo maana mkandarasi wa kichina imemsikitisha sana mpaka akalia ni jinsi gan hatuwajali na kuwakumbuka watu kama hao,tunakumbuka kununua magari ya kifari kwa viongoz wetu tu inasikitisha sana maisha yao ni magumu lakini walishaitumikia Tanzania kwa kuijenga vilivyo

Anonymous said...

Kwa kweli inasikitisha sana,hadi mkandarasi wa kichina amelia jinsi gani vyenyew hatuwajari wakufunz wetu.maisha wanayoishi mabaya wakati waliitumikia Tanzania vilivyo

Anonymous said...

Jambo la kutojali watu pamoja na raslimali kwa viongozi wa Tanzania imekuwa ni jambo la kawaida. Pengine ni kutokana na sheria ya kinga ktk kuwashitaki viongozi hasa wa ngaz za juu serikalin na hata kupelekea kulindana.

Mchina kalia kuona wastaafu wana hali mbaya lakin waTZ hasa viongoz ha2shituki rejea kitendo cha kigogo wa TANESCO kuagiz sanduku misumari Ulaya kwa mbilioni ya fedha. Kwao huyo Mchina viongoz wa aina hizo hata mtu yeyote angeishia kunyongwa.

WaTZ nasi 2ngenakili sheria hiyo na kuwaondolea kinga viongozi, 2ngeweza kusogea kama sio kutoka hapo 2lipo.

Lefodi Paulo Sanga said...

Hii ndo Tanzania inayowajali wastaafu,tunaomba mshua alisikie hili na alifanyie kazi. Awakumbuke wapiganaji hawa kwa kuwapa fulsa ya maisha bora kwa utendaji na si kwa maneno.