Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, November 26, 2011

ZAIDI YA MILIONI 80 ZATUMIKA UNUNUZI WA PIKIPIKI ZA WATENDAJI KATA 36‏

JUMLA ya pikipiki 36 zikiwa na thamani zaidi ya milioni 80 zimetolewa kwa maafisa watendaji wa Kata 36 zilizopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Mbeya.




JUMLA ya pikipiki 36 zikiwa na thamani zaidi ya milioni 80 zimetolewa kwa maafisa watendaji wa Kata 36 zilizopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Akikabidhi pikikipi hizo  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya evince Balama amewataka watendaji hao kutumia vifaa hivyo kwa malengo husika na kutambua kuwa huo ni mkopo ambao watapaswa kurejesha kwa kipindi cha miaka mitatu mfululuzo.

Alisema, mradi huo ambao huko chini ya halmashauri umelenga kuboresha huduma za wananchi katika Kata na vijiji hivyo kuwaonya watendaji hao kutotumia kwa shughuli zao binafsi.

Alisema, serikali inategemea ushirikiano mkubwa baina ya watendaji na wananchi katika kuwasaidia na kukamilisha shughuli za maendeleo ili kuhakikisha ujenzi wa shule za Sekondari za Kata unakamilika.

“Serikali inatambua mchango mkubwa kwa watendaji pamoja na wananchi na kutambua changamoto zilizokuwa zikiwakabili ikiwa ni uchelewaji wa kufika katika vituo vya kazi hivyo kusababisha wananchi kutotendewa haki,”alisema

Aidha, Mkuu huyo alikemea tabia ya baadhi ya watendaji kujisahau katika majukumu yao ya kazi na kuwa kero kwa wananchi kutokana na kujikita zaidi kwenye ulevi wa kupindukia.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Ethanas Kapunga, alikemea tabia ya watendaji kujiingiza kwenye siasa hali inayopelekea kudhorotesha shughuli mbalimbali za maendeleo.

Pia, alisema mradi huo ulipitishwa kwa wakati na umelenga kutekeleza malengo ya kazi kwa watendaji wa Kata katika kuhakikisha shughuli mbalimbali za maendeleo zinatekelezwa kwa wakati.

“Nisingependa kusikia mtendaji akitoa sababu za kutoendelea shughuli za maendeleo na kutowasilisha taarifa zitakazo itajika kwa wakati muafaka ikiwa na kutokuwepo kwenye viyuo vya kazi kwa kisingizio cha usafiri,

No comments: