Add caption
BAADHI ya Waandishi wa Habari mkoani
Mbeya wanatarajia kufanya ziara (Study Tour) Nchi jirani ya Malawi kwa lengo la
kujifunza mambo mbali mbali.
Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi
ya safari hiyo iliyofanyika juzi kwenye Hotel ya Mbeya Peak, Mwenyekiti wa
Kamati ya safari hiyo, Ulimboka Mwakilili ambaye pia ni Raisi Mstaafu wa UTPC
alisema safari hiyo itaanza Agost 17, mwaka huu.
Alisema kutokana na urefu wa safari hiyo
ambayo haimlazimishi mtu, kila anaevutiwa anapaswa kuchangia gharama za usafiri
pamoja na chakula na malazi.
Alisema kima cha chini ni shilingi Laki
mbili (200,000/=) kwa kila mtu mchango ambao mwisho wa kupokelewautakuwa Agost
8, mwaka huu.
Alisema safari hiyo ni muhimu kwa waandishi
wa habari Mkoa wa Mbeya kutokana na manufaa ya kukutana na kujua mazingira ya
kazi ya waandishi wa Habari wan chi jirani ya Malawi ikiwa ni pamoja na kujenga
mahusiano mema.
Aliongeza kuwa wanahabari hao wakiwa
Nchini Malawi watafanya shughuli mbali mbali ambazo hakuzitaja kwa kile
alichodai ratiba maalumu inapangwa kwa ushirikiano na wenyeji ambao ni
waandishi wa habari nchini Malawi.
Kwa upande wake Mratibu wa Safari hiyo,
Venance Matinya, alisema ni vema ikaeleweka kuwa safari hiyo haiwahusu
Wananchama wa Klabu ya waandishi Mkoa wa Mbeya(mbeya press club) bali ni kwa
mwandishi yeyote aliyetayari.
Alisema safari hiyo imeasisiwa na
waandishi wa habari wakongwe hapa nchini na Mkoa wa Mbeya na waliowahi kushika
nyadhifa mbali mbali za uongozi kwenye Klabu.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment