ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini,
Dk. Donald Mwanjoka amekabidhi vyandarua 100 katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa kanisa
hilo.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi
vyandarua hivyo, Askofu huyo alisema zoezi hilo linafanyika kutokana na Kanisa
hilo kitaifa kuanzishwa Mkoa wa Mbeya pamoja na sherehe kufanyika kitaifa Mkoa
wa Mbeya.
Awali akitoa utambulisho katika hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Mwenyekiti wa
Kamati ya Huduma za Jamii wa TAG, Dk. Leonard Maboko, ambaye pia ni Mkurugenzi
wa NMR, alisema mbali na askofu huyo kukabidhi vyandarua hivyo katika hospitali
hiyo pia Maaskofu wengine wametawanyika katika Hospitali za Jiji la Mbeya na Wilaya
ya Mbeya kwa ajili ya kukabidhi vyandarua hivyo.
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya
Mkoa wa Mbeya Dk. Gloria Mbwile, Alilipongeza Kanisa kwa kutimiza miaka 75
tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania pamoja na kutambua umuhimu wa huduma za
jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina aliwashukuru Kanisa kwa msaada na kuongeza kuwa
kitendo hicho ni kutekeleza mfumo wa serikali wa kuzishirikisha sekta binafsi
katika mfumo wa (PPP).
Aliongeza kuwa hivi sasa serikali
inakabiliwa na kutekeleza mpango wa mileniawa kupunguza vifo vya mama na mtoto
kutokana na Malaria hivyo kitendo cha Kanisa kutoa msaada huo ni kuisaidia
Serikali kwa kutoa vyandarua bure tofauti na serikali ya kutoa kwa mfumo wa
hati Punguzo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment