Mratibu wa Mradi, Fadhili Nswilla(katikati) akitoa mada kwa washiriki wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Washiriki wa Semina ambao miongoni mwao ni waandishi wa habari na wadau.
*************
KATIKA kuhakikisha Serikali inadhibiti na kukabiliana na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kila mwananchi ametakiwa kushiriki kuwalea watoto hao.
Wananchi watashiriki moja kwa moja katika kuwalea watoto hao kupitia mradi mpya wa pamoja tuwalee ambapo utaanza kufanya kazi kuanzia ngazi ya Kaya hadi Kata.
Hayo yalielezwa jana na Mratibu wa mradi wa Pamoja tuwalee unaofadhiliwa na PACT, Fadhili Nswilla, wakati wa semina elekezi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Nswilla alisema lengo la semina hiyo ni kutambulisha mradi mpya unaomlenga kila mwananchi kuchukua jukumu la kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuanzia ngazi ya kaya.
Alisema mradi huo ni mpya katika mpango mkakati wa awamu ya pili wa Serikali ambao unamwezesha kila mwanajamii jinsi ya kuweza kuwahudumia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu tofauti na mpango wa kwanza ambao misaada mbali mbali ilikuwa ikitolewa na wafadhili.
Alisema katika mradi huo umelenga kubadili mtazamo wa wananchi ambao walizoea kupokea misaada ya vitu kwa ajili ya watoto na kuwajengea uwezo katika ngazi ya kaya hadi Kijiji ili kuweza kujitegemea na kuweza kuwahudumia watoto hao pasipo kutegemea msaada.
Aliongeza kuwa kwa kuanzia katika Jiji la Mbeya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali matatu yamegawana Kata 18 kila Shirika ili kuhakikisha wanatembea na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mradi wa pamoja tuwalee.
Aliyataja mashirika hayo kuwa ni pamoja na Kanisa la Anglican , Shirika la pact na Shirika la NICE ambayo kwa pamoja yataweza kuzifikia kata 36 za Jiji la Mbeya na kutoa elimu kwenye vikundi kwa ushirikiano wa Madiwani, Watendaji na viongozi wa Serikali za Mitaa.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment