- APATA FURSA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUONGEA NA WAKAZI WA ENEO HILO
- VIJANA WALIOCHUKUA KADI ZA CCM SIKU CHACHE ZILIZOPITA WAZISALIMISHA
Vijana wa Mtaa wa Tonya - Ituha walimpokea Mbunge wao kuelekea Tonya
Msafara wa Mbunge kuelekea Mtaa wa Tonya
Mbunge alilakiwa na kikundi cha ngoma cha vijana
Mbunge Joseph Mbilinyi akicheza ngoma baada ya kuwasili mtaa wa Tonya
Msafara wa Mbunge ukaelekea kufungua Ofisi ya CHADEMA -Tonya
Mh. Joseph Mbilinyi akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Tonya ambaye naye ameshiriki katika kuikamilisha
Hapa Mbunge Sugu akijiandaa kuzindua ofisi
Akisaini kitabu cha wageni kuonyesha kuwa ofisi imefunguliwa rasmi
Baada ya zoezi hilo Mbunge alipelekwa na diwani kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa daraja katika mtaa wa Tonya
Hapo Mbunge Joseph Mbiliyi akiongea na wakazi wanaoishi kandokando ya daraja hilo
Pia Mbunge alipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ambapo madarasa mapya yamejengwa
Joseph Mbilinyi "Sugu" hapo akiwa katika mkutano wa hadhara katika Mtaa huo wa Tonya
Wazee nao walikuwepo kusikiliza Mbunge akielezea shuhuli za kimaendeleo zilizofanyika jimboni
Mmoja wa Kijana maarufu wa eneo hilo ambaye alichukua kadi ya CCM siku chache zilizopita alirudisha kadi kwa Mbunge na kuelezea kuwa alichukua kwa kuwa alikuwa akihitaji shilingi 5,000 zilizokuwa zinagawiwa na CCM kwa vijana ili wagawiwe kadi hizo za CCM
Wazee wakimshukuru Mbunge kwa kuwa mwakilishi wao mwema katika jimbo la Mbeya mjini
Vijana wakikabidhiwa kadi za CHADEMA na mbunge wao
Vijana wakiwemo ambao walirudisha kadi za CCM siku chache zilizopita wakiwa wanaonyesha kadi zao za CHADEMA walizokabidhiwa na Mbunge
Wananchi wakionge na Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya mkutano wa hadhara
Baadaye Mbunge Sugu alimalizia na kikao cha ndani na baadhi ya wakazi wa Tonya ambapo pia alipata fursa ya kupokea maoni na maswali na pia alitolea ufafanuzi mambo mbalimbali
No comments:
Post a Comment