Chunya yazidi kukua kimaendeleo
Wilaya ya
Chunya inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 48 katika bajeti ya mwaka
2014/2015 kwa miradi ya huduma na maendeleo.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Charles Mwakalila alipokuwa akiongea na
mwandishi wa Mbeya yetu ofisini kwake hivi karibuni.
Baadhi ya
miradi iliyopewa kipaumbele ni miradi ya maji,elimu,miundo mbinu ya barabara na
ujenzi wa uwanja wa michezo utakaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 8.2.
Mwakalila
amesema kuwa mapato ya Bajeti hiyo yatatokana na vyanzo mbalimbali kama vile
tumbaku,kilimo madini na ruzuku kutoka serikalini.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wananchi kuwekeza
katika wilaya hiyo kwani hivi sasa imepiga hatua katika mawasiliano ya simu na
barabara kuu ya Chunya/Mbeya inayojengwa kwa kasi kubwa.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Tutasubiri mkamilishe hivyo vipaumbele vyenu maana wewe si wakwanza kutamka. Maji ni tatizo kubwa sana chunya (mf. Makongolosi). miundo mbinu yake ni ya zamani sana.
Post a Comment