Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na
unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya Mbeya
Vijini wameuawa na wananchi katika mapambano makali pembezoni mwa Mlima Mbeya.
Jambazi la kwanza lilitambuliwa
kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi Juhudi Jijini Mbeya ambaye aliuwa
na wananchi baada ya kupata taarifa ambapo walifanikwa kumzingira na kufanikiwa
kumkamata eneo la Msangamwelu Kata ya Mshewe.
Juhudi za wananchi ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka
majambazi wengine ziliendelea na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili
waliotambuliwa kwa majina ya Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani Tabora na
Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta Jijini Mbeya.
Hata hivyo juhudi za wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine
wawili waliosalia wakiwa na bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika
msitu mnene kupandisha Mlima Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi jingine
lililokuwa na silaha na mfuko wa risasi ambapo wananchi walilidhibiti ndipo
alirusha silaha na risasi msituni na kuanza kupambana na wananchi kwa
kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata na katika mapambano hayo jambazi
hilo liliuawa kwa kutumia silaha za jadi na mawe.
Jambazi mwingine alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha
Ihombe kwa ushirikiano na wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Ikukwa na
Msangamwelu ambalo pia lilipambana na wananchi hao na Askari majira ya saa tano
asubuhi Mei 13 mwaka huu ambapo lildhibitiwa na kuuawa.
Mapambano hayo ya hatari katika msitu huo yalikuwa yakifanyika kwa
tahadhari kubwa kutokana na kutojua idadi yao na aina ya silaha walizo nazo na
mpaka sasa silaha na risasi havijapatikana katika msitu huo.
Baadhi ya majambazi kabla ya kuuawa imedaiwa kujihusisha na matukio ya
ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe,Iringa
na Morogoro ambapo walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi waliojitolea kupambana na
majambazi hao kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambayo
imeanza kuzaa matunda na kufanikiwa kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya
ili Mbeya iwe na amani muda wote.
Wakati wa uporaji majambazi hayo yapatayo matano yalipanga mawe
barabarani eneo la Msangamwelu na kufanikiwa kupora pesa,simu na pikipiki aina
ya SANYA yenye namba T 682 CHT ambayo baadaye waliitelekeza msituni walipokuwa
wanafuatiliwa na wananchi.
Majambazi hao walimjeruhi Dereva wa roli hilo aliyefahamika kwa jina la
Sephen Mgogo ambaye amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi na miili ya
majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya ambapo wawili
kati yao hawajatambuliwa.
Jeshi la Polisi waliondoka Kijiji cha Ihombe majira ya saa moja na nusu
usiku baada kazi ngumu ya kubeba miili ya majambazi hao mwendo wa masaa matano
kwa miguu kutoka uneo la mapambano.
Na Ezekiel Kamanga
wa Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment