Baba mzazi Kolinel Mushin kushoto akimsikiliza mkewe kwa makini baada ya mama huyo kufika kijijini kwao
Mtoto Selemani Kolineli Mushin(Miezi
kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
amerejea salama Kijijini baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa na
matatizo ya mdomo sungura.
Mtoto huyo alifichwa ndani baada ya
kuzaliwa na kutakiwa kurudi Hospitali ya Wilaya ya Chunya miezi sita baadaye
lakini Baba Mzazi wa mtoto huyo aitwae Kolineli Mushin akikataa kumpeleka
Hospitali akidai huo ni mpango wa Mungu.
Mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya mtoto
huyo kukutwa na mwandishi wa Mbeya yetu na kuwashauri wazazi wa mtoto ndipo walipokubali
kumpeleka Hospitali ambapo dhamana hiyo ilichukuliwa na Afisa Ustawi wa jamii
Anna Geleta la kusafirishwa hadi Hospitali ya CCBRT.
Selemani baada ya kupokelewa katika
Hospitali ya CCBRT alifanyiwa upasuaji na kurekebishwa mdomo ambao ulikuwa
ukimpa shida wakati wa kula na kupumua kwa shida na aliruhusiwa kutoka
Hospitali Mei 15 Mwaka huu na kurejea Mbeya Mei 17 ambapo gharama za safari ya
kwenda na kurudi na matibabu kugharamiwa na CCBRT.
Kwa upande wake Baba mzazi Kolinel Mushin
na Mkewe Yohana Kolineli wameishukuru Mbeya yetu blog, Serikali na Asasi ya CCBRT kwa
kufanikisha matibabu ya mtoto wao ambapo wao walidhani kuwa ugonjwa huo
usingetibika.
Aidha walimshukuru msamaria mwema Osward
Mwailomo aliyetoa taarifa kwa mwanahabari na Mwenyekiti wa Kijiji cha Igundu
kwa ushirikiano wake hata kufanikisha upasuaji wa mtoto na hali yake inaendelea
vema.
Selemani atafanyiwa upasuaji wa pili mwezi Mei
mwakani katika Hospitali hiyo ya CCBRT ambapo gharama zote hutolewa na
Hospitali hiyo.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment