|
John Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya kupigwa kisha kunyimwa chakula na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Mwanahawa Nassoro(32)mkazi wa Airport Kata ya Iyela. |
|
Bibi Lahel Mbembela akilia kwa uchungu mara tu baada ya kumwona mtoto John |
|
Bibi Lahel Mbembela akimkabidhi Muuguzi kiasi cha shilingi 10,000/ kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo |
|
Afisa Ustawi wa Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Mwanahawa hivyo aliandika barua ya msamaha wa matibabu ili atibiwe bure ambapo alilazwa Machi 13 Jioni baada ya Madaktari kufanya uchunguzi wa kina. |
|
Joseph Mwaisango akimjulia hali mtoto John kulia ni Msamaria mwema Grolia Kaguo ndiye aliyejitolea kumhudumia mtoto John
|
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya kumshikilia Mwanamke mmoja, Mwanahawa Nasoro(32) Mkazi wa Airport
Mkoani hapa akituhumiwa kumtesa na kumnyanyasa mtoto wa kaka yake,
Hatimaye mtoto huyo aanza kupatiwa matibabu.
Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la
John Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada
ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya kupigwa kisha kunyimwa
chakula na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Mwanahawa Nassoro(32)mkazi
wa Airport Kata ya Iyela.
Baada ya mtuhumiwa kukamatwa Mtendaji wa
mtaa Henry Chaula aliomba msaada kwa wasamaria wema kumkimbiza Hospitali mtoto
ili kuokoa maisha kutokana na kuzorota kwa afya kulikotokana na kipigo na
ukosefu wa lishe.
Katika Hospitali ya Rufaa alipokelewa na
Afisa Ustawi wa Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa na kitendo
kilichofanywa na Mwanahawa hivyo aliandika barua ya msamaha wa matibabu ili
atibiwe bure ambapo alilazwa Machi 13 Jioni baada ya Madaktari kufanya
uchunguzi wa kina.
Hata hivyo Msamaria Mwema Groria Kaguo
alijitolea kulazwa pamoja na mtoto huyo kwa lengo la kusimamia
huduma huku Madaktari na wauguzi wakifanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya
mtoto huyo kutokana na sehemu kubwa ya mwili wake umeathirika na majeraha
yaliyotokana na viboko.
Baadhi ya wasamaria wema Kikiwemo kituo
cha Radio cha Bomba FM Mbeya, Gazeti la Jamboleo Mbeya na Mtandao wa Mbeya Yetu
wameanza kugharamia fedha za matibabu hayo ambapo dawa alizoandikiwa
hazipatikani Hospitali ya Rufaa na kulazimu kununua kwenye duka nje ya
Hospitali.
|
Mtoto Baraka Joseph(02) akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa mbeya |
|
Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama lishe anayefahamika kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa Nonde Jijini Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa baada ya mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya matibabu. |
|
Wakati huo huo,Mtoto mwenye umri wa
miaka miwili jinsi ya kiume ambaye alitelekezwa katika kituo kikuu cha mabasi
Jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ngiri.
Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama
lishe anayefahamika kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa
Nonde Jijini Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa
baada ya mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya
Rufaa kwa ajili ya matibabu.
Baada ya uchunguzi wa Madaktari
walibaini mtoto Baraka Joseph(02) kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ngiri hivyo
waliamua kumfanyia upasuaji Machi 12 mwaka huu ambapo hivi sasa anaendelea vema
na amelazwa wadi 6 ya watoto katika hospitali ya Rufaa na hali yake inaendelea
vema.
Mama Sunche amemtaka mama aliyetelekeza
mtoto huyo afike kumchukua kwani uwezo wake ni mdogo kiuchumi sasa shughuli
zake zimekwama kutokana na muda mwingi kutumika kumhudumia mtoto pia kama mzazi
wake aliona kuwa tatizo la ugonjwa ndiyo kikwazo asihofu kwani sasa mtoto
ametibiwa.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi
kutowatelekeza watoto kutokana na ugumu wa maisha au mafarakano katika ndoa
bali wanandoa watatue migogoro ya ndoa kwa hekima na uadilifu ili kupunguza
wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Baadhi ya mahitaji yanayohitajika kwa
mtoto huyo na pamoja na nguo,chakula na mahitaji mengine madogo madogo kama
sabuni na mafuta.
Aidha amewaomba wasamaria wema
kumsaidia chochote ili aweze kujikimu kimaisha kwani hakutarajia kupata mtoto
kwa muda huu na Asasi zinazohudumia watoto kutokuwa na mwitikio wowote hivyo
kuachiwa jukumu la kulea mtoto na ametoa wito mwenye kuguswa awasiliane nae kwa
namba za simu 0753732025.
Vitendo vya kutelekeza watoto na
unyanyasaji wa watoto ni miongoni mwa matukio yaliyoshika kasi hivi sasa katika
mkoa wa Mbeya licha ya kuwepo kwa Taasisi nyingi zianazopiga vita zikiwemo
TAMWA na TGNP.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment