Rashidi Mkwinda aliyeshika nafasi ya pili katika kipengere cha Uandishi wa Habari za Mazingira. |
Festo Sikagonamo nafasi ya pili katika Kipengere cha Uandishi wa Habari za Utawala |
Gordon Kalulunga aliyeshinda katika kipengere cha Uandishi wa Habari za Afya na Uzazi. |
MTANDAO wa Kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com
na Kampuni nzima ya Tone Multimedia Company Limited(TMCL) unawapongeza
waandishi wa Habari walioibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha umahiri wa
uandishi wa Habari (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT).
Mbali na kuwapongeza waandishi wa Nchi
nzima waliobahatika kuchaguliwa kushiriki kinyang’anyiro hicho na wengine
kuchaguliwa katika nafasi mbali mbali Mtandao huu unawapongeza wawakilishi wa
Mkoa wa Mbeya katika Tuzo hizo kwa kuibuka washindi katika Fainali iliyofanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.
Waandishi hao ni pamoja na Rashidi
Mkwinda aliyeshika nafasi ya pili katika kipengere cha Uandishi wa Habari za
Mazingira, Festo Sikagonamo nafasi ya pili katika Kipengere cha Uandishi wa
Habari za Utawala Bora sambamba na Gordon Kalulunga aliyeshinda katika
kipengere cha Uandishi wa Habari za Afya na Uzazi.
Washindi hao waliowakilisha vema Mkoa wa
Mbeya kwa pamoja walitunukiwa Vyeti, Ving’amuzi pamoja na madishi ya DSTV kila
mmoja.
Mtandao huu unatoa pongezi na wito kwa
wanahabari wengine kuiga mfano wa kujituma katika kuandika habari za kijamii
ili hatimaye na wao waje kuibuka washindi katika mashindano yajao ili kuboresha
utendaji kazi na weledi wa taaluma ya habari katika Mkoa wetu wa Mbeya.
Aidha baadhi ya Wadau wa Habari Mkoani
hapa ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walitofautiana kuhusu utaratibu
unaotumika kuwapata washindi ambapo baadhi yao walipongeza na wengine wakiponda
kwa madai kuwa utaratibu huo umepitwa na wakati na kwamba wahusika wanapaswa
kubadilika.
Walisema kawaida mtu hawezi kuomba
kupewa au kuchaguliwa kuwa mshindi katika nafasi yoyote isipokuwa ni kwa wadau
wanaofuatilia habari hizo ndiyo wanaoweza kuchagua ama kumteua mfanyakazi bora
na mahiri wa uandishi kutokana na mguso wa habari anazoziandika.
Waliotolea mfano namna anavyopatikana
mfanyakazi bora katika taasisi katika kilele cha siku ya wafanyakazi duniani
kuwa hupigiwa kura na wafanyakazi wenzie na siyo wao kupeleka maombi na
kuongeza kuwa hata katika kumpata mchezaji bora pia hupigiwa kura na mashabiki
na sio wachezaji kutuma maombi.
Walisema suala hilo linaweza kuwa na
viashiria vya rushwa kwa baadhi ya washiriki kutaka kujaribukuwashawishi
wahusika ili wawachague kuwa washindi kutokana na utaratibu unaotumika kutoenda
na wakati.
Walienda mbali zaidi kuwa pia mitandao
ya kijamii inapaswa kuhusishwa katika vinyang’anyiro hivyo kwa kuwa ndicho
chanzo cha habari zinazochapishwa kwenye baadhi ya magazeti na vituo vya Redio
ambavyo huombea tuzo habari walizozitoa kwenye mitandao.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment