HALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi Mkoani
Mbeya imelalamikiwa kwa kuhodhi zaidi ya shilingi milioni 254 zilizotolewa na
serikali kuu kwa ajili ya miradi mbalimbali katika mji wa Tunduma kabla ya
kuganywa kuwa Halmashauri mbili.
Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa
mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma, Elias Cheyo, alipokuwa akitoa taarifa kwa
Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kata ya Tunduma, Hemed Stephen, alipofanya
ziara ya kukagua miradi mbali mbali.
Cheyo alisema kutokana na kutopelekwa
kwa fedha hizo kumesababisha kukwama kwa ujenzi wa vyumba 21 vya madarasa ya
shule mbalimbali katika kata hiyo.
Baadhi ya shule zilizokumbwa na adha
hiyo ni pamoja na Shule ya msingi Mkombozi na Mwaka ambazo zinakabiliwa na
changamoto kubwa za msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani.
Cheyo alisema kuwa kukosekana kwa fedha
hizo kunawakatisha tamaa wazazi ambao wameweza kujenga madarasa hadi
mtambaapanya wakati jukumu la serikali ni kupaua na kumalizia sakafu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Momba,Aidan Mwanshiga alisema ruzuku hiyo
ilitumwa Halmashauri mama ya Mbozi ambayo inapaswa kutoa fedha hizo kila mwezi
lakini haijafanya hivyo kwa mwaka mmoja sasa.
Mwanshiga alisema kuwa wametafuta fedha
nyingine kutokana na vyanzo vya ndani ili kupunguza adha hiyo ya upungufufu wa
madarasa ili ifikapo mwezi marchi watoto wote wawe madarasani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Ambakisye Minga alipoulizwa kuhusiana na tuhuma
hizo alisema kuwa hana maelezo kuhusiana na jambo hilo atafutwe Mkurugenzi wa
Halmashauri yeye ndiye mwenye dhamana ya kujibu masuala ya fedha za Hamashauri.
Hata hivyo juhudi za kumpata Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Charles Mkombachepa kupitia
simu yake ya kiganjani zilifanikiwa ambapo alijibu kuwa yupo kwenye
kikao.
|
No comments:
Post a Comment