WADAU mbali mbali na wasamaria wema
wamezidi kujitokeza kumpa msaada wa hali na Mali,Aida Nakawala(25) mkazi wa
kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, aliyejifungua watoto
wanne mapacha kwa mkupuo(Quadruplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya.
Misaada hiyo imeongozana ikiwa ni siku
moja baada ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Vanesa pamoja na Mbeya yetu
kutoa misaada mbali mbali ambapo leo Kampuni ya Arif Electronic nayo imeguswa.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo pamoja na
familia yake, Faizar Kasamia, baada ya kuguswa na hali ya Mama huyo ametoa vitu
vya aina mbali mbali vyenye thamani ya Shilingi Laki tatu.
Vitu alivyotoa ni pamoja na Nguo,Maziwa
(Lactogen), Mafuta, Sabuni na Nepi.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Mungu awabarik na awazidishie wote waloguswa kumsaidia huyu dada, MESHACK MWAKILEMBE pande za ilombe apa, be blessed mr. bloger
Post a Comment