Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 12, 2012

MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA MJINI ASEMA HAYUKO TAYARI KWENDA KUHOJIWA NA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA UCHOCHEZI KWENYE MIKUTANO YA HADHARA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mbeya Mjini John Mwambigija,
akiongea na waandishi wa habari katika hotel ya mbeya peak

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti huyo anahitajika  polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa chadema Mbeya mjini



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mbeya Mjini John Mwambigija, amesema hayuko tayari kwenda kuhojiwa na polisi  kuhusu tuhuma zinazomkabili za kutoa kauli za uchochezi kwenye mikutano ya hadhara.

Kauli zinazodaiwa kutolewa na Mwenyekiti huyo zilitolewa kwenye mikutano ya wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa CHADEMA katika Jimbo la Lupa  Wilayani Chunya  kwenye opareshini ya Chadema ya Twanga kotekote (NATO).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti huyo anahitajika  polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Alisema, moja ya tuhuma zilizolifikia jeshi la polisi kutoka kwa wananchi  ni kwamba kiongozi huyo amekuwa akitoa maneno ya uchochezi huku akiwahamasisha wananchi kufanya vurugu zilizoambatana na uharibifu wa mali za watu.

Alisema, kiongozi huyo akiwa katika mikutano, wananchi hueleza matatizo yanayowakabili amekuwa akiwahamisisha wakazi hao kudai haki kwa kufunga barabara na hata kuchoma nyumba za viongozi kama walivyofanya uharibifu wa mali za askari katika Kata ya Lupa Tinga-Tinga.

“Kiongozi huyu amekuwa  akiwahamasisha wananchi kuchoma matairi ikiwa na kufunga barabara pindi wanapotaka kutatuliwa madai yao kwa serikali jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa sheria, hivyo  jeshi la polisi linamtaka kiongozi huyo kufika kituoni ili kutoa maelezo ya tuhuma zinazomkabili,”alisema.

Alisema, kazi ya askari ni kupokea malalamiko kwa maandishi na kuyafanyia kazi na kwamba katika utekelezaji askari huchukua maelezo ya pande zote mbili na ndio maana kiongozi huyo anahitajika kwenda kutoa maelezo ya upande wa pili.
 Aidha, Kwa upande wa Mwambigija alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza opareshini yao, alisema yeye yupo tayari kwenda kituo cha polisi endapo atakuwa na makosa ya jinai lakini kwa masuala ya kisiasa hawezi kufanya hivyo na endapo wataendelea kumfuatilia patachimbika kupitia nguvu ya umma.
 Alisema, kazi ya jeshi la polisi ni kufanyia kazi taarifa wanazozitoa na si kumwita yeye kwenda kutoa maelezo na kwamba wanachokifanya wao kwa wananchi ni kutoa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.
 “Polisi tunawasaidia kufanya kazi na mimi sitaenda polisi kwa sababu tu za kisiasa kama ni hivyo CHADEMA kinawanasheria wengi ambapo tumekuwa tukikamatwa mara kwa mara na tunashinda kesi hizo,”alisema
Mwambigija  na kuongeza  kuwa chama cha CHADEMA kinanguvu ya umma isiyotumia silaha bali maneno hivyo hatuwezi kufundishwa kutumia maneno matamu majukwaani.
 Alisema, kitendo cha polisi kuwaita kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo eti kwa sababu walitoa maneno makali na kwamba hilo ni jambo ambalo  hawezi kulifanya kamwe bali kama ingekuwa ni kosa la jinai.
 Hivi karibuni Mjumbe wa mkutano Mkuu Taifa kupitia chama cha Chadema, Edo Mwamalala alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kumchukulia hatua Mwenyekiti huyo wa Chadema wilaya kutokana na kauli zake za uchochezi anazozitoa kwenye mikutano ya hadhara.

No comments: