Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 5, 2012

SAKATA LA KUTOFUNGWA KWA HARUSI, KAMATI YANUIA KUMFIKISHA MZAZI WA BIBI HARUSI MAHAKAMANI.

Mwemyekiti wa kamati ya harusi iliyovunjika Bwana Jeremia Mahenge akifungua sherehe hiyo bila kuwepo maharusi ukumbini

Wanakamati wakimsikiliza mwenyekiti wao jinsi mambo yalivyoharibika

Bwana harusi Mwalimu Gervas ametoa tamko mbele ya wanakamati kuwa hayupo tayari kumwoa tena binti huyo, kutokana kitendo cha kushirikiana na mzazi inadhihirisha kuwa hakuwa na upendo wa dhati kwake.

Waalikwa wakicheza wenyewe bila ya maharusi kamati ya sherehe hiyo imemtaka mzazi wa bi harusi kurejesha gharama za sherehe hiyo

Wazazi wa binti pamoja na washenga wa pande zote mbili katika picha ya pamoja


Kamati iliyokuwa ikishughulikia harubi ya Mwalimu Gervas Mwashihamba Makambuya (29), imeazimia kumfikisha mahakamani mzazi wa Bibi harusi, Daktari Akimu Mwalukosya wa Kijiji cha Mbigili Mwakaleli Wilaya ya Rungwe.

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bwana Jeremia Mahenge maarufu kwa jina la Vamponji, katika Ukumbi wa Vamponji  akidai sababu iliyotolewa na mzazi wa bibi harusi ya kuwa bwana harusi hakutuma usafiri wa kumchukua binti yao haziridhishi, kwani wangepewa taarifa mapema.

Mbali na hilo amesema wamesikitishwa na kitendo cha mshenga wa bwana harusi kwa kuwasaliti kwani hakuonekana siku ya alhamisi iliyopita huko kijijini kwao alipokuwa akiangwa binti Ikupa Akimu (29), kwa kile kilichotafsiriwa kuwa alirubuniwa na mzazi wa bibi harusi ili kuvuruga harusi hiyo.

Aidha katika Kikao hicho Bwana harusi Mwalimu Gervas ametoa tamko mbele ya wanakamati kuwa hayupo tayari kumwoa tena binti huyo, kutokana kitendo cha kushirikiana na mzazi inadhihirisha kuwa hakuwa na upendo wa dhati kwake.

Hata hivyo ameishukuru kamati ya maandalizi ya harusi yake kwa kitendo cha kiungwana walichokifanya na juhudi kubwa kutaka kufanikisha harusi hiyo lakini hali ikawa tete kutokana na wakwe zake kutokuwa radhi binti yao kuolewa naye.

Mwalimu Gervas ameongeza kuwa atawasiliana na washenga wake ili kurudishiwa mahali zake, huku kamati imepanga kuwasiliana na Mwanasheria kutokana na kitendo hicho ili kuangalia uwezekano wa kurejeshewa gharama zilizotumika kuandaa sherehe hiyo iliyo gharimu zaidi ya shilingi milioni 4,300,000.

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya

No comments: